Pages

Thursday, 28 June 2012

SERIKALI ITOE TAMKO JUU YA KILICHOMSIBU DK. ULIMBOKA

Dk. Ulimboka akiwa na majeraha baada ya kushambuliwa
Mbunge wa Nzega, Dk Khamis Kigwangala ameitaka Serikali kutoa majibu fasaha kuhusu kilichomtokea Dk Stephen Ulimboka akieleza kuwa kilichomtokea kiongozi huyo wa madaktari kinasikitisha. Dk Kigwangala alisema hayo jana alipozungumza na gazeti hili kuhusu tukio lililomkuba Dk Ulimboka.

Alisema kuwa ni muhimu kwa Serikali kufanya hivyo kwa kuwa Dk Ulimboka alikuwa katika harakati za kudai haki za madaktari ambapo kabla hawajafikia azma yao  amekutwa na jambo la kusikitisha.

 “Ukimwangalia picha zake huwezi kumtambua, tumefikia mahali kitu kama hiki kinatokea, inasikitisha sana. Kuna haja kwa Serikali kuthibitisha kuwa haijahusika kwa tukio hilo kwani taarifa silizosambaa zinaeleza kuwa imehusika,”alisema Dk Kigwangala. Alisema ni lazima Serikali iwajibike kwenye suala hilo ingawa haamini kama inaweza kufanya tukio kama hilo.

Dk Kigwangala alisema taarifa zilizopo ni kwamba Daktari huyo alipigiwa simu na mtu wa Serikali ili kuangalia namna gani wanaweza kuzungumzia kusitisha mgomo huo. Akizungumzia historia ya Dk Ulimboka alisema kuwa  ni mtu mwenye msimamo mkali na asiyependa kuyumbishwa waliyekutana Chuo Kikuu cha Tiba Muhimbili (MUHAS) mwaka 1998 walipokwenda kusomea udaktari.
Alisema kabla ya Dk Ulimboka kujiunga na MUHAS alitokea Shule ya Sekondari Mzumbe ambapo alikuwa amesomea mchepuo wa Sayansi(PCB).

UHISPANIA YATINGA FAINALI ZA EURO 2012 NCHINI POLAND & UKRAINE

game ilipigwa kwa dakika 120
Mabingwa watetezi Uhispania wamefuzu kuingia fainali ya Euro 2012, baada ya kuishinda Ureno magoli 4-2, kupitia mikwaju ya penalti, baada ya muda wa kawaida wa dakika 90 na dakika 30 za ziaida kumalizika kwa timu hizo mbili kushindwa kufungana.
Bao la mwisho la mikwaju ya penalti kwa Uhispania lilitiwa wavuni na Cesc Fabregas, na kuwapa wenzake matumaini ya kutetea ubingwa wao kikamilifu, watakapocheza aidha na Ujerumani au Italia katika fainali ya Jumapili.
Fabregas, ambaye ni kiungo cha kati wa timu ya Barcelona, alipiga mkwaju ambao baada ya kugonga mwamba upande wa kushoto, ulitambaa wavuni, na ikawa ni tiketi ya Uhispania kufanya mipango ya kusafiri hadi Kiev, Ukraine, kwa fainali.
Mchezaji wa Ureno, Bruno Alves, alielekea kuwa na wasiwasi, na kushindwa kufunga mkwaju wake, baada ya mpira kugonga mwamba, na Ronaldo, akiwa amepangwa na timu yake katika nafasi ya tano kwa wapigaji penalti, hakupata hata nafasi ya kutimiza wajibu huo.
Wengine waliokosa kufunga kupitia mikwaju ya penalti ni mchezaji wa Ureno, Joao Moutinho, wakati kipa wa Uhispania, Casillas, alipoweza kuokoa kwa kuruka upande wa kkulia.
Awali mchezaji wa Uhsipania Xabi Alonso naye alikosa kutumbukiza wavuni mkwaju wa penalti, licha ya kwamba ulikuwa ni mkwaju wa kasi na uliopigwa kwa nguvu, lakini kipa Rui Patricio akauzuia.

Wednesday, 13 June 2012

DI MATTEO ASAINI MKATABA WA MIAKA MIWILI KUINOA CHELSEA

Kocha aliyechukua mikoba kwa muda baada ya kufukuzwa kwa Andres Villa Boas Chelsea, Di Matteo amesaini mkataba wa miaka miwili kukinoa kikosi hicho tokea jijini London.

Di Matteo, 42 alichukua jukumu la kuinoa Chelsea kwa mkataba wa muda mfupi baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo kufukuzwa kazi. Di Matteo alishinda vikombe viwili akiwa kama kocha wa muda wa Chelsea, Kombe la FA Cup na lile la Klabu Bingwa barani Ulaya.

Mchezaji huyo wa Italy pia Chelsea mapema jumatano hii baada ya kutangazwa kuwa kocha wa kudumu amesema "Nina furaha sana kuchaguliwa kama kocha mkuu wa kikosi cha kwanza"

"Wote kwa pamoja tulipata mafanikio makubwa msimu uliopita kitu kilichoweka historia kwa klabu hii kubwa duniani. Lengo letu ni kuendeleza kile tulichokipata na nimejiandaa vizuri kwa ajiri ya maandalizi ya msimu ujao" aliongeza kusema Di Matteo

Uwezo wa Di Matteo umeweza kuonekana baada ya kuifanya Chelsea kuwa klabu ya kwanza toka jiji la London kuweza kushinda kombe la UEFA Champions League.

MATUMAINI YA MASHABIKI WA UHOLANZI KABLA YA MECHI NA GERMANY


Mechi imemalizika kwa Uholanzi kupokea kipigo cha 2-1 toka kwa Wajerumani a.k.a roho ya paka, magoli ya Germany yakifungwa na Super Mario Gomezi huku lile la kufutia machozi toka kwa Uholanzi likifungwa na Van Persie

Tuesday, 12 June 2012

TFF YATOA RUKSA YONDANI KUCHEZA YANGA MSIMU UJAO

Yanga wakimtambulisha Yondani baada ya kusaini mkataba

Utata wa usajili wa Kelvin Yondani unaelekea kupata majibu mapema baada ya kuthibitika kuwa ataichezea Yanga msimu ujao. 

Mmoja wa wajumbe wa kamati mmojawapo ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) aliithibitishia Mwanaspoti jana Jumatatu kuwa Yondani atacheza Yanga msimu ujao baada ya kugundua udanganyifu uliofanyika Simba. 

"Hapa tuwe wa kweli. Simba wanasema walimsainisha Yondani Desemba mwaka jana, tunajua kuwa Yondani alikuwa na matatizo na Simba wakati huo angesaini vipi mkataba mpya?" Alihoji mjumbe huyo wa TFF. 

Mjumbe huyo alisema Simba wanaonekana kushindwa mapema katika kesi hiyo kwa sababu kama wangekuwa wanamtaka Yondani wangemsainisha kabla hajaingia miezi sita ya mwisho na mkataba wake ungesajiliwa TFF. 

"Hivi unadhani Simba wangekuwa wanamtaka Yondani wangesubiri mpaka mkataba wake uishe?" Alihoji. 

"Huyu sisi tuna taarifa kuwa alisaini Simba baada ya timu kurejea kutoka Algeria katika Kombe la Shirikisho. Ila walichokifanya ni kurudisha nyuma tarehe ya usajili ili ionekane amesajili Desemba. 

"Hata kama amesajili Desemba bado walichelewa kwa sababu wakati huo tayari Yondani alikuwa amebakiza mkataba wa miezi sita, hivyo alikuwa huru kusaini klabu yoyote. " 

Mwanaspoti ilipomuuliza Yondani atacheza timu gani msimu ujao alisema: "Kwa mazingira yote hayo ni dhahiri atacheza Yanga kwa asilimia mia." 

Familia ya Yondani 
Kaka mkubwa wa Kelvin Yondani ambaye pia ni wakala wa mchezaji huyo, Sunday Patrick ameridhia beki huyo kwenda Jangwani. 

Sunday aliiambia Mwanaspoti wiki iliyopita kuwa: "Sisi kama familia kwa moyo mmoja tupo na Yondani katika uamuzi wake, cha msingi yeye amefuata sheria na hana mkataba wowote na Simba ndio maana hata sisi tumempa baraka za kwenda Yanga, pia viongozi wa Simba wanapaswa kufahamu kuwa mchezaji huyu bado ni mdogo na anatafuta maisha hivyo wamuache afanye uamuzi wake." 

Kauli ya Yondani 
Yondani ambaye awali alidai kusaini Simba, Alhamisi iliyopita aliikana kauli hiyo na kusema amesaini Yanga. 
"Nimesaini Yanga, nawatakia kila la kheri Simba." 

Yondani amelamba Sh.30 milioni kutoka Yanga na atakuwa akilipwa mshahara wa Sh 800,000 ingawa kuna taarifa kuwa ameongezewa na atakuwa akilipwa Sh milioni moja kwa mwezi huku ikidaiwa Simba ilipanga kumpa Sh 25 milioni na angelipwa mshahara wa Sh 800,000. 

Kanuni ya TFF 
Kanuni ya 43 ya TFF ya masharti ya mikataba kati ya wachezaji na klabu kifungu cha 3 kinasema; " Klabu inayotarajia kuingia mkataba na mchezaji wa kulipwa haina budi kuiarifu klabu yake ya sasa kwa maandishi kabla ya kufanya makubaliano na mchezaji huyo wa kulipwa. 

Mchezaji wa kulipwa atakuwa huru tu kuingia mkataba na klabu nyingine iwapo mkataba wake na klabu yake ya sasa umekwisha au utakwisha baada ya miezi sita. Uvunjaji wowote wa sharti hili utastahili vikwazo vinavyofaa."

Tafsiri ya kanuni 
Kutokana na kanuni hiyo, Yondani alikuwa huru kufanya mazungumzo au hata kusaini mkataba na klabu yoyote tangu Desemba mwaka jana kwa sababu mkataba wake ulikuwa umebakiza miezi sita kwani umekwisha Mei 31 

Monday, 11 June 2012

MCHEZAJI WA ZAMANI WA ENGLAND NA KLABU YA EVERTON GORDON WEST AFARIKI AKIWA NA MIAKA 69

West mwenye jezi ya kijana akionyesha cheche zake
Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya England na klabu ya Everton, Gordon West afariki dunia akiwa na miaka 69 baada ya kusumbuliwa na maladhi kwa muda mrefu.

West alikaa Goodison Park kwa miaka 11 huku akicheza michezo zaidi ya 400 na alifanikiwa kushinda mataji 2 ya ligi mwaka 1963 na 1970, pia kombe la FA mwaka 1966.

Everton ilimsajili Gordon West kwa kitita cha pound za Uingereza 27,000 kutoka Blackpool na kuweka rekodi ya goli kipa kusajiliwa kwa pesa nyingi kwenye ligi ya England.

Pia kipa huyo alipata kushinda vikombe vitatu akiwa na England, na alikuwa moja kati ya wachezaji wa kikosi cha England kilichoshika nafasi ya tatu kwenye michuano ya Ulaya mwaka 1968. Hata hivyo baada ya miaka miwili West alikataa kwenda Mexico kushiriki kombe la Dunia na timu ya taifa ya England kwa kisingizio cha kutaka muda wa kutosha kukaa na familia yake.

Gordon West pia alipata kucheza timu jirani na Everton, Tranmere Rovers

NIGERIAN POLICE RESCUE ABDUCTED FOOTBALLER OBODO


Mchezaji aliyekuwa ametekwa nyara Christian Obodo
Nigerian police have rescued Christian Obodo without the payment of a ransom demanded by his abductors.


Officers tracked his alleged abductors to Isoko, just outside Warri, on Sunday, where they found Obodo and arrested some suspects.
The midfielder was abducted by unknown gunmen near the oil city of Warri in southern Nigeria on Saturday.
The kidnappers had issued a ransom demand for nearly US$200,000 (£129,000).
Obodo, who was on loan at Italian side Lecce from rivals Udinese last season, was driving alone early on Saturday morning when he was abducted.
It is not the first time a footballer has been kidnapped in Nigeria.
International defender Onyekachi Apam was kidnapped by armed men who took his car before releasing him.
Nornu Yobo, elder brother of Everton defender Joseph, was famously kidnapped in 2008 in oil-rich Port Harcourt.
Nornu was released after 10 days but it was never made clear whether a ransom was paid.
Last year, the father of Chelsea midfielder John Mikel Obi was also seized in Jos, north-central Nigeria.
Nigerian police, however, rescued Micheal Obi senior from his abductors days later.

source: www.bbc.co.uk/football

MJUE MCHEZAJI WA KWANZA MWENYE ASILI YA AFRIKA KUCHEZA SOKA LA KULIPWA

Arthur Wharton
Shirikisho la Soka la Kimataifa, Fifa, limemtunuku Tuzo ya Mwanasoka wa Kwanza mwenye asili ya Afrika kucheza soka ya kulipwa, Arthur Wharton.


Fifa ilitoa tuzo hiyo kwa mchezaji huyo aliyekuwa akiichezea Darlington ya England. Shughuli hiyo ya tuzo ilifanyika Makao Makuu ya Fifa mjini Zurich.

Rais wa Fifa, Sepp Blatter, alisema kuwa shirikisho lake limefanya hivyo kuonyesha kuwa hakuna ubaguzi wa rangi katika soka.

"Hii ni siku muhimu kwa Fifa," alisema.

"Tunafanya kazi kupinga ubaguzi. Soka inaunganisha watu, inaleta watu karibu, na tunamtunuku kupitia Arthur Wharton Foundation," alisema Blatter. 

"Alikuwa mwanasoka wa kwanza mwenye asili ya Afrika kucheza Ligi Kuu England lakini tunajiuliza, imechukua muda gani hadi mchezaji mweusi kuitwa kwenye timu ya taifa ya England, ni kama miaka 100."

"Mwanasoka huyu tayari anafahamika Wembley na FA imechanga pauni 20,000 kama heshima yake Darlington katika mfuko wake wa maendeleo ya soka.

Wharton alikuwa raia wa Gold Coast (sasa Ghana), alikwenda England mwaka 1884, akiwa na miaka 19. Alikuwa na mpango wa kucheza soka katika klabu ya Methodist iliyoko Cleveland College, Darlington.

Mwaka 1886 alikuja kuwa mkimbiaji wa mita 100 na alishinda mbio hizo. Mwaka mmoja baadaye alishinda mbio za baiskeli zilizokuwa zikishindanwa kutoka Preston hadi Blackburn.

Uwezo wake katika michezo ulionwa na Klabu ya Darlington ambayo ilimsajili kama golikipa na aliidakia kuanzia 1885 hadi 1888 na kuwa Mwafrika wa kwanza kucheza soka ya kulipwa England. Alizichezea pia Preston North End, Stockport County na Sheffield United.

Mfanyabiashara na mmiliki wa Darlington FC, Shaun Campbell alimsajili Wharton kwa zaidi ya miaka mitano.

"Ni wazi kutambuliwa kwake na Fifa ni sehemu ya mafanikio na kunaupa nguvu mfuko wa Arthur Wharton," anasema Blatter.

Sunday, 10 June 2012

RESULTS: TANZANIA 2 - 1 GAMBIA


Vijana wa Kim Poulsen timu ya soka ya Tanzania maarufu kama Taifa Stars imepigana kufa na kupona leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya timu ya Taifa ya Gambia.

Gambia ndio waliokuwa wa kwanza kufunga goli lililowekwa kimiani mnamo dak. 7 ya mchezo na Ceesay, Taifa Stars walijitajidi kadri ya uwezo wao kusawazisha bao hili lakini kosakosa nyingi langoni mwa Gambia hazikuzaa matunda hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.

Dakika ya 60 kipindi cha pili, Shomari Kapombe aliisawazishia Taifa stars kufuatia klosi nzuri iliyopigwa na Erasto nyoni ikitokea winga ya kulia.

Watanzania wakiwa na matumaini ya kupata ushindi walizidi kulisakama lango la Gambia mara baada ya kusawazisha goli lakini Wagambia hao walikuwa na safu nzuri ya ulinzi iliyowapa tabu sana vijana wa Tanzania.

Mnamo dakika ya 84 beki wa Gambia alinawa mpira kwenye eneo la hatari kufuatia klosi hatari iliyopigwa na Mbwana Samatta. Erasto Nyoni alipiga kwa ustadi mkubwa penati hiyo na kuiandikia Stars bao la 2 na la ushindi.

Mpaka sasa Stars inashika nafasi ya pili iliwa na pointi 3, pointi moja nyuma ya vinara Ivory Coast wenye pointi 4 baada ya kutoka sare hiyo jana na Morroco. Gambia wao wanashika mkia wakiwa na pointi 1 baada ya kutoa sare mchezo wao wa kwanza dhidi ya Morroco.

BREAKING NEWS: WAZIRI WA USALAMA NCHINI KENYA AFARIKI KWA AJALI YA HELKOPTA


Waziri Saitoti
Waziri wa Usalama wa ndani Profesa George Saitoti na Naibu wake Orwa Ojode wamefariki dunia katika ajali ya helikopta ya polisi iliyotokea leo asubuhi katika eneo la Kibiku, karibu na mji wa Ngong takriban kilometa ishirini kutoka mji mkuu wa Nairobi.
Abiria wote sita, wakiwemo marubani wawili na walinzi wa mawaziri hao waliokuwa kwenye helikopta hiyo wamefariki dunia na miili yao kuteketezwa kwa kiasi cha kutoweza kutambulika.
Kilichosababisha ajali hiyo bado hakijabainika.
Bwana Saitoti na maafisa wengine wa juu katika wizara ya usalama wa ndani walikuwa wakielekea katika eneo la Sotik kwa mkutano wa usalama. Saitoti alikuwa miongoni mwa wanasiasa mashuhuri nchini Kenya waliokuwa wakipania kugombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao.
Walioshuhudia ajali hiyo wamesema waliona helikota hiyo ikizunguka angani kabla ya kuanguka katika msitu wa Ngong.
Polisi wamezingira eneo la ajali hiyo na kamishna wa polisi Mathew Iteere aliyepo katika eneo la ajali anatarajiwa kutoa taarifa kamili kuhusiana na ajali hiyo.
Ajali hiyo ya helikopta imetokea katika siku ambapo Kenya inaadhimisha miaka minne tangu kutokea ajali ya ndege iliyowauwa mawaziri wengine wa serikali, Kipkalya Kones na Lorna Laboso.

ARSENE WENGER AITAHADHALISHA ENGLAND KUELEKEA MCHEZO DHIDI YA UFARANSA


Arsene Wenger

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger anaamini kufungwa kwa Ufaransa au England kwenye mchezo wa kwanza wa Kundi D utaozikutanisha timu hizo utapoteza matumani yao Euro 2012.

England itavaa Ufaransa mjini Donetsk hapo Jumatatu mechi ambayo Wenger anaamini itaamua hatma ya kundi hilo lililokuwa na nyingine Sweden na wenyeji wenza Ukraine.

Wenger alisema hayo wakati wa mahojiano na tovuti ya Arsenal (www.arsenal.com) kuwa England wana kibarua kigumu zaidi baada ya kuwakosa nyota wake kadhaa wakiwemo Wayne Rooney ambaye amefungiwa kucheza mechi mbili za kwanza za nchi hiyo.
"Mechi ya ufunguzi kati ya England na Ufaransa na kukosekana kwa Rooney, unaweza kusema ni mchezo ambao hatakiwi kupoteza," alisema Wenger.

"Kwanini? Kwa sababu hutaweza kurudi kwenye mstari wa ushindani kutokana na presha kubwa kutoka kwa mashabiki wa nchi zao wanaotaka kuona timu yao ikishinda tu.
"Mechi hiyo itaamua hatma ya kundi lote. Kama ikimalizika kwa sare 0-0, hapo kundi litakuwa wazi kwa wote, lakini kama moja atafungwa atakuwa wamejifungulia njia ya kutolewa kwa sababu Ukraine itaifunga moja ya nchi hizo mbili na Sweden ni timu ngumu kufungika."

Wenger anaamini mchezo wa kwanza wa England ndiyo utakaoamua hatma yao wakiwa na kocha wao mpya Roy Hodgson.

"England watamkosa Rooney, wana kocha mpya na hawajakaa pamoja... ni vigumu kuwategeneza na kuwa timu kwa haraka," alisema.

"Unaweza kufanikiwa au hapana? Hiyo itajulikana baada ya mechi ya kwanza.
"Faida pekee kwa England ni kuwa na kocha mzoefu Hodgson aliyewahi kufundisha timu ya taifa na mwenye uzoefu na mashindano haya na mwenye kuwafahamu vizuri wachezaji wa England.


"Kwa sasa England bado wanaangaika kujenga kujiamini na kama wakifanikiwa kufanya hilo, basi wataweza kupata matokeo mazuri."

Wakati huohuo; Wenger anaamini Ufaransa ina uwezo wa kurudia mafanikio yake ya Euro 2000, lakini kama wachezaji wake wakiweka kado mawazo mabaya yaliyowakutaka kwenye fainali za Kombe la Dunia 2010.

"Wachezaji wa Ufaransa wanaweza kutwaa ubingwa wa fainali hizi," alisema Wenger.


"Lakini bado hawajiamini vya kutosha kwa sababu ya tukio lililowakuta Afrika Kusini. 

Mategemeo kwa Ufaransa ni madogo kwa sababu ya jambo hilo, lakini wana uwezo.

"Wana wachezaji nyota kama Benzema, (Franck) Ribery, (Samir) Nasri. Kama wakiandaliwa vizuri kisaikolojia naweza kuwashangaza wengi kwenye michuano hiyo."

Saturday, 9 June 2012

OKWI KWENDA ORLANDO PIRATES YA AFRIKA KUSINI




 Emmanuel Okwi wa Simba ameitwa kuichezea Orlando Pirates ya Afrika Kusini itakapocheza na Newcastle ya England katika michuano ya Kombe la Vodacom jijini Johannesburg. 

Orlando Pirates inataka kutumia michuano hiyo ya Vodacom ambayo hushirikisha timu tatu kumjaribu Okwi na iwapo atafanikiwa itampa mkataba wa kuichezea msimu ujao. 

Michuano hiyo msimu huu inashirikisha timu tatu ambazo ni Orlando Pirates, Kaizer Chiefs na Newscastle. 

Mchezo huo kati ya Orlando Pirates na Newcastle utafanyika Julai 14 mwaka huu jijini Johannesburg na kuonyeshwa na vituo vya televisheni vya Supersport kwa Afrika na Skysports kwa Ulaya. 

"Hata hivyo ni muhimu benchi la ufundi likamuona Okwi kabla ya mechi hiyo. 

Nimezunguma na benchi la ufundi wamesema baada ya mapumziko, wachezaji wanatakiwa kurejea kambini Juni 25. Hata hivyo watashauri siku ambayo wanamtaka Okwi jijini Johannesburg," alisema Felix Sapao, ambaye ni wakala wa wachezaji mwenye ofisi yake Malawi. 

"Awali Orlando walikuwa wakimtaka Kazadi Mutombo wa AS Vita ya Congo kwa majaribio, lakini nimejitahidi kumshawishi mwenyekiti wa Orlando Pirates, Khoza wamwangalie kwanza Emmanuel Okwi na amekubali. 

Amenipa masharti kwamba ninunue tiketi ya ndege ya kuja na kurudi ya Okwi, nimekubali kufanya hivyo," alisema Sapao. 

Sapao alisema ni vyema Okwi akianza kucheza Orlando Pirates kabla ya kufikiria kwenda Ulaya kwani atapata masilahi mazuri akitokea Afrika Kusini. 

"Kama mambo yakienda vizuri Simba watafaidika sana kwa sababu kutakuwa na kipengele ambacho kitawafanya wapewe asilimia 30 iwapo atauzwa kwenda Ulaya kama zinavyofanya TP Mazembe na Orlando Pirates ambazo huwauza wachezaji kwa dola za Marekani 1.5 milioni," alisema Sapao. 

Hivi karibuni, Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage alisema wamepata ofa kutoka nchi tatu ambazo mchezaji huyo anatakiwa. 
Alizitaja nchi hizo kuwa ni England, Serbia na Australia. 

Okwi amekuwa katika kiwango cha hali ya juu msimu uliopita na anakumbukwa vizuri kwa kuhusika katika mabao matano ambayo waliifunga Yanga katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Bara.

source: http://mwanaspoti.co.tz

SUAREZ: ANDREA PIRLO IS BETTER THAN XAVI HERNANDEZ

Pirlo na Xavi wakipambana kwenye moja ya mechi 
Former Spain international Luis Suarez believes Andrea Pirlo is a more complete player than Xavi Hernandez.

Reigning champions Spain take on Italy in their opening match of Euro 2012 on Sunday looking to take charge of a group also containing Croatia and Republic of Ireland.

Xavi and Pirlo are expected to play key roles for their teams in the game, and former Barcelona and Inter Milan star Suarez, who was inspirational in helping Spain to European Championship glory in 1964, believes that the Juventus star has greater all-round quality.

“I have to point out first that Italy is my home, but my heart is Spanish,” Suarez told La Gazzetta dello Sport. “These are two champions with a great sense of positioning and know how to pick the right moment to start a move. They both have experience and technique.

“They are similar players, but in my view Pirlo has more of a range, can spread the play more and seek the longer passes. It’s true Xavi gets fewer passes wrong, but that’s because he plays them short and at most will pass 20 metres to the wings, so there are fewer risks. Andrea aims for more difficult passes and that brings with it the risk of getting it wrong sometimes.

“Andrea strokes the ball better, which is why he’s also better with free kicks and scores a few goals”Luis Suarez explains his preference for Andrea Pirlo over Xavi
“At the end of the day, I think Pirlo is a more complete player than Xavi. Andrea strokes the ball better, which is why he’s also better with free kicks and scores a few goals. He’s also more determined in the tackle, whereas Xavi is light and just uses his positioning to defend.“If they were to exchange teams, they would both do well, but the Catalan seems built to play for Barcelona and Spain. The Italian is more adaptable and can speed up the pace of his team-mates too. This is why I believe Pirlo is more important for Cesare Prandelli than Xavi is for Vicente Del Bosque.” Xavi, meanwhile, has said he expects Italy to take an attacking approach on Sunday. “Italy has changed its system,” he told Marca and Adidas. “Now the team wants to play the ball more with a packed midfield diamond, and Andrea Pirlo is the outstanding player in that area of the pitch. “They also have two great strikers like Mario Balotelli and Antonio Cassano. They no longer hold back like in the catenaccio years. Now they try to play the ball and take the initiative, as they have the players for that. We are going to see an entertaining spectacle tomorrow. It’s not going to be one of those games in which they are closed up and Spain has the ball constantly.” source: espnfc.com

Thursday, 7 June 2012

TAARIFA KUTOKA TFF


WAZIMBABWE KUCHEZESHA TAIFA STARS, GAMBIA
Waamuzi kutoka Zimbabwe ndiyo watakaochezesha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia hatua ya makundi Kanda ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Gambia itakayochezwa Juni 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) mwamuzi wa kati atakuwa Ruzive Ruzive. Waamuzi wasaidizi ni Salani Ncube na Edgar Rumeck wakati mwamuzi wa akiba ni Norman Matemera.

Kamishna wa mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni ni Fanie Wallace Mabuza kutoka Swaziland wakati mtathmini wa waamuzi (referee assessor) ni Ali Baligeya Waiswa.

Waamuzi hao watawasili nchini kesho (Juni 8 mwaka huu) saa 1.20 usiku kwa ndege ya Kenya Airways wakati Kamishna wa mechi hiyo atawasili siku hiyo hiyo saa 12.50 jioni kwa ndege ya South African Airways. Mtathmini wa waamuzi atatua pia Juni 8 mwaka huu saa 7.55 mchana kwa ndege ya Kenya Airways.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inaendelea na mazoezi leo saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam chini ya Kocha Mkuu Kim Poulsen.

GAMBIA KUWASILI LEO USIKU
Timu ya Taifa ya Gambia (The Scorpions) ambayo awali ilikuwa iwasili nchini leo (Juni 7 mwaka huu) saa 1.40 asubuhi sasa itawasili leo saa 9.20 usiku kwa ndege ya Kenya Airways tayari kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars.

The Scorpions ilipaswa kubadili ndege Dakar, Senegal jana usiku lakini kukawa na ucheleweshaji (delay), hivyo ikashindwa kuwahi Nairobi, Kenya ambapo ingeunganisha kwa ndege ya alfajiri kuja Dar es Salaam.

Kikosi cha timu hiyo chenye wachezaji 22 wakiwemo tisa wanaocheza mpira wa kulipwa nje ya nchi hiyo kitafikia kwenye hoteli Sapphire iliyopo Mtaa wa Lindi na Sikukuu eneo la Kariakoo.

Wachezaji walioko katika msafara huo ni Musa Camara, Abdou Jammeh, Momodou Futty Danso, Lamin Basmen Samateh, Ousman Koli, Pa Saikou Kujabi, Mustapha Kebba Jarju, Yankuba Mal Ceesay na Demba Savage.

Wengine ni Saihou Gassama, Alieu Darboe, Momodou Ceesay, Pa Modou Jagne, Tijan Jaiteh, Bubacarr Sanyang, Christopher Allen, Musa Yaffa, Sulayman Marr, Mamut Saine, Hamsa Barry, Ali Sowe, Omar Colley na Saloum Faal.

PROGRAMU YA MAZOEZI YA GAMBIA

IJUMAA JUNI 8
01.00 asubuhi Mazoezi- Uwanja wa Karume
10.00 jioni   Mazoezi- Uwanja wa Taifa

JUMAMOSI JUNI 9
04.00 asubuhi  Mkutano na Waandishi wa Habari- Ukumbi wa TFF
10.00 jioni  Mazoezi- Uwanja wa Taifa

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

KOCHA MPYA WA VILLARREAL AFARIKI DUNIA KABLA YA KUANZA KIBARUA CHAKE

Manolo Preciado
Manolo alikifundisha kikosi cha Sporting Gijon kwa miaka 6
 Kocha mpya aliyechaguliwa na timu ya Villarreal kwa ajiri ya kikinoa kikosi chake kuanzia mwanzoni mwa msimu ujao Manolo Preciado amefariki dunia asubuhi ya leo baada ya kusumbuliwa na tatizo la moyo [heart attack].

Kocha huyo wa zamani wa Sporting Gijon amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 54, gazeti la Marca la nchini Uhispania limelipoti.

Preciado, ndo kwanza alikuwa amekubali ofa ya kikinoa kikosi cha Villarreal kuanzia msimu ujao na alitegemea kutambulishwa rasmi kwa mashabiki na vyombo vya habari ijumaa ya kesho, siku moja kabla ya kifo chake.

Habari kwenye tovuti ya klabu ya Villarreal inasomeka "Kocha Manolo Preciado amefariki usiku wa manane mjini Valencia kutokana na shambulio la moyo"

"Villarreal inaeleza kwa masikitiko makubwa kuondokewa na mtu huyu na inatoa pole kwa familia yake na ndugu zake pia"


Tuesday, 5 June 2012

OFFICIAL: RONALDINHO ASAINI MKATABA MPYA NA KLABU YA ATLETICO MINEIRO YA NCHINI BRAZIL

Ronaldinho - Flamengo
Dinho kazini
 Baada ya kubwaga manyanga kwenye klabu yake ya Flamengo kutokana na madai ya mshahara wake mapema week iliyopita, kiungo wa kimataifa wa Brazili amesaini mkataba wa kuichezea timu ya Atletico Mineiro pia ya nchini Brazili.

Taarifa zilizothibitishwa na klabu hiyo ya Atletico Mineiro zimeeleza kuwa mchezaji huyo amesaini mkataba utakao mfanya acheze kwenye timu hiyo hadi mwishoni mwa mwaka huu.

Ronaldinho, 32 mara baada ya kusitisha mkataba wake na timu ya Flamengo alihusishwa na taarifa za kwenda kucheza soka lake nchini  Uchina kwenye klabu ya Guangzhou Fuli pia alihusishwa na kuhamia timu ya Palmeiras.

Lakini taarifa za Gaucho kusaini mkataba na Atletico Mineiro zinaondoa uvumi huo uliomhusisha mchezaji huyo mara baada ya kubwaga manyanga timu ya Flamengo.


Monday, 4 June 2012

JOHN BARNES: FERDINAND HANA HAKI YA KUICHEZEA ENGLAND

Rio Ferdinand katika moja ya mechi na timu ya Taifa ya England
John Barnes na David Pleat wameunga mkono uamuzi wa kocha wa timu ya Taifa ya England Roy Hodgson wa kutomjumuisha kwenye kikosi chake mchezaji mkongwe wa Manchester United Rio Ferdinand.

Mapema week hii baada ya kocha Roy kuthibitisha kuwa beki wa kati wa Chelsea Gary Cahill hataweza kuiwakilisha nchi yake kwenye michuano ya Euro 2012 inayotarajiwa kuanza mapema mwezi huu, kocha huyo aliamua kumuita kwenye kikosi chake kinda Martin Kelly ilikuziba pengo la beki huyo.

Kitendo hicho kilionekana kuwakera baadhi ya wadau wa soka wanaomsupport beki wa Man United Rio Ferdinand.

Mwakilishi wa beki huyo [Jamie Moralee] amemtuhumu kocha Roy pamoja na shirikisho la soka nchini Uingereza kuwa limemkosea heshima mchezaji huyo kwa kutomjumuisha kwenye kikosi chake kitakachoshiriki michuano ya Euro 2012.

Lakini suala hili limechukua sura mpya baada ya David Pleat kushangazwa na kauli hiyo ya Moralee huku akiita kauli hiyo kuwa iko nje ya majukumu [out of order].

Naye John Barnes amesema "Soka la kimataifa la kila mmoja hufika kikomo, kumuacha mtu kwenye kikosi cha timu ya taifa si kumkosea heshima"

"nilicheza michezo 79 nikiwa na timu ya taifa na niliachwa nje ya kikosi kwa sababu muda wangu wa kuichezea timu ya taifa ulikuwa umekwisha. Suala lilibaki ni kumuunga mkono kocha" Barnes aliendelea kusema.

Rio amekwisha cheza michezo 81 na timu ya taifa ya England , aliachwa kwenye kikosi cha kwanza cha Roy kabla ya kuachwa tena baada ya Cahill kupatwa na majeraha yaliyomfanya kocha huyo kumuweka kando ya kikosi chake kitakachoshiriki micchuano ya Euro 2012.


YUSUPH MANJI ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UENYEKITI YANGA

Yusuph Manji



Habari za kuaminika kutoka Makao Makuu ya klabu ya Young African Sports Club zinaeleza ya kuwa mwanachama maarufu na mpenzi mkubwa wa timu hiyo Yusuph Manji amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa klabu hiyo.

Kuchukua fomu kwa Manji kunathibitisha uvumu uliokuwa umezagaa juu ya nia ya tajiri huyo kugombea nafasi ya Uenyekiti klabuni hapo. Ingawa Manji hakueleza kama fomu hiyo ni ya kwake, watu waliokaribu na mdhamini huyo wa zamani wa Yanga wameeleza kuwa jamaa ana nia ya kugombea.

Kwa habari zaidi endelea kufuatilia mtandao huu.



ROGER FEDERER ASONGA MBELE UFARANSA


Roger Federer
Roger Federer
Katika mashindano ya mchezo wa Tennis ya Ufaransa, Roger Federer amefuzu kushiriki robo fainali kwa ushindi wa 5-7, 7-5, 6-2, 6-4 dhidi ya David Goffin wa Ubelgiji.
Mchezaji huyo anayeshikilia namba ya tatu kwa ubora Duniani sasa atapambana na mshindi wa pambano la Juan Martin del Potro wa Argentina na Tomas Berdych wa Jamhuri ya Czech kuania nafasi ya kushiriki nusu fainali.
Wakati huo huo mchezaji namba moja Duniani, Novak Djokovic amependezesha mchuano wa kufuzu kuingia robo fainali licha ya mpinzani wake Andreas Seppi kuongoza seti mbili za mwanzo 4-6, 6-7 lakini aliweza kutumia umahiri wake na kushinda seti za mwisho 6-3, 7-5, 6-3.
Mchezaji huyo bora hata hivyo alionekana mchovu asiyekua katika hali ya ushindani akitishia kua anayeweza kuanguka kwenye hatua hii.
Djokovic
Novak Djokovic
Djokovic, anayetazamia kukamilisha idadi ya Vikombe vya mashindano ya kiwango cha 'grand slam' kwa kushinda Ufaransa, atachuana na mshindi kati ya Stanislas Wawrinka na Jo-Wilfried Tsonga.
Katika mashindano ya wanawake mchezaji namba moja Victoria Azarenka alikiri kua kila alichojaribu kukifanya kilikwenda kombo uwanjani na hivyo kuondolewa kwenye mashindano ya mwaka huu ya Ufaransa na Dominika Cibulkova.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alifululiza ushindi mara 26 mwanzoni mwa mwaka 2012 ikiwa ni pamoja na kushinda ngao yake ya kwanza kwenye kinyanganyiro cha Australia.
Wiki hii nzima Azarenka ahakuonyesha kiwango cha mchezo aliouonyesha mapema mwaka huu ikiashiria angeweza hata kutupwa nje mapema.

Sunday, 3 June 2012

NEMANJA VIDIC EYES SEASON OPENER FOR UNITED


Manchester United defender Nemanja Vidic is hopeful of being fit for the start of the 2012-13 season.
Nemanja Vidic's knee twists under Basel's Marco Streller
Nemanja Vidic's knee twists under Basel's Marco Streller
Vidic, 30, has been sidelined since December after damaging knee ligaments which ruled him out for the remainder of the campaign.
Red Devils boss Sir Alex Ferguson recently confirmed he does not expect the Serbian to be ready for the club's pre-season tour, but Vidic is positive about his recovery.
He said in the Sun: "I can now run and do some things on the pitch which is better for me psychologically because for the last four months it's been every day in the gym, which is hard.
"But the worst part is behind me. I can look forward to the second half of the rehabilitation and work more on my fitness. Hopefully, I'll be fit for the big kick-off."

RONALDINHO ABWAGA MANYANGA FLAMENGO

Gaucho katika moja ya mechi alizochezea Flamengo
Mchezaji wa zamani wa Fc Bacelona na kiungo mchezeshaji wa timu ya taifa ya Brazil Ronaldinho Gaucho amebwaga manyanga kwenye timu ya Flamengo aliyokuwa akiichezea baada ya mgogoro wa muda mrefu kuhusu malipo ya mshahara wake.

Ronaldinho amekuwa kwenye vita ya maneno na Flamengo kwa muda mrefu kuhusiana na madai yake hayo huku mchezaji huyo akieleza kutokuwa na amani klabuni hapo baada ya kufanyiwa vitendo visivyo vya kiungwana [ Rubro-Negro ] kwenye mchezo dhidi ya Internacional.

Mapema alhamisi hii Flamengo walipinga ripoti zilizoeleza kuwa kiungo huyo wa kimataifa wa Brazil yuko huru, hata hivyo hatua hiyo ilipelekea Ronaldinho, 32 kuchukua hatua zaidi za kisheria kwa kuishitaki timu yake akidai zaidi ya Euro milioni 16 za mshahara wake, bonasi na haki za picha [image rights]. Labour Court ya mjini Reo de Janeiro ilitoa iliyosikiliza kesi hiyo ilitoa maamuzi yenye manufaa dhidi ya Gaucho [gaucho alishinda kesi].

Nalo shirikisho la soka nchini Brazili (CBF) lilikuwa likisubiri uamuzi wa mahakama ili kumfanya Ronaldinho awe mchezaji huru.

Hata hivyo Vice-President wa Flamengo ameeleza kupata taarifa za hukumu ya mahakama hiyo ya Labour na kueleza nia ya klabu ya Flamengo kukata rufaa dhidi ya maamuzi ya mahakama.

KALOU & DROGBA WAPELEKA KILIO TAIFA STARS

Stars katika maandalizi kabla ya mechi na Ivory Cost

Tanzania imeanza vibaya kampeni zake za kucheza Fainali za Kombe la Dunia Brazil 2014 baada ya kufungwa mabao 2-0 na Ivory Coast.

Katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Felix Houphouet Boigny, Stars ilijitahidi kucheza kandanda la kawaida kwa pasi za kawaida tofauti na ilivyotarajiwa.

Ikiwa ni mtihani wa pili kwa kocha wake, Kim Poulsen baada ya mchezo wa kwanza wa kirafiki na Malawi kutoka 0-0, Stars ilipoteana dakika ya tisa tu na kufungwa bao kirahisi lililowekwa kimiani na Solomon Kalou.

Kalou aliwapiga chenga mabeki watatu wa Stars baada ya kuunasa mpira mguuni kwa Kelvin Yondan aliyezubaa kuuondosha akiwa ndani ya eneo la hatari.

Baada ya bao hilo, Stars ilijipanga upya na kuelekeza mashambulizi langoni kwa wapinzani wao na dakika ya 14, Aggrey Moris alipiga mpira wa adhabu uliogonga mwamba lakini hata hivyo, wachezaji wa Ivory Coast walikuwa makini kuondosha.

Katika dakika ya 22, Didier Drogba naye aligongesha mwamba kwa mpira wa adhabu iliyosababishwa na Morris baada ya kumkwatua Kalou akiwa nje kidogo ya eneo la hatari. Morris alionyeshwa kadi ya njano kwa faulo hiyo.

Dakika mbili baadaye, ushirikiano wa Mbwana Samatta na Morris aliyepanda kusaidia mashambulizi nusura uzae bao lakini hawakuwa makini.

Beki huyo anayechezea Azam alipiga kombora lililotokana na mpira wa adhabu baada ya Mwinyi Kazimoto kukwatuliwa ndani ya eneo la hatari na Tiote lakini hata hivyo likatoka nje.

Stars iliendelea kuliandama lango la wapinzani wao na katika dakika ya 36, ilipata kona tatu mfululizo zilipigwa na Amir Maftah lakini hata hivyo zilikuwa tasa. Dakika ya 40 hadi kumalizika kipindi cha kwanza, Stars ilicheza pasi za hapa na pale na kuwachanganya Ivory Coast.

Kipindi cha pili kilianza taratibu na hata hivyo Stars iliyokuwa na uchu nusura ipate bao dakika ya 62 lakini kichwa cha Samatta hakikulenga lango, kabla ya Gervinho kujibu dakika mbili baadaye baada ya kumtoka Maftah.

Kocha wa Ivory Coast, Sabri Lamouchi alifanya mabadiliko kwa kuwatoa Gervinho na Tiote na nafasi zao kuchukuliwa na Kader Keita na Konnan Didier.

Stars ilipata pigo dakika ya 63 baada ya beki wake wa kati, Morris kulimwa kadi nyekundu kwa kumkwatua Kalou ikiwa ni kadi ya pili ya njano. Kuona hivyo, Kim Poulsen alimtoa Salum Aboubakar na nafasi yake kuchukuliwa na John Boko.

Dakika ya 70, Didier Drogba aliipatia Ivory Coast bao la pili kwa mpira wa kichwa baada ya kuunganisha krosi ya Keita. Kuona hivyo, Poulsen alimtoa Boko na kumuingiza Erasto Nyoni kwa ajili ya kuimarisha safu ya ulinzi. 

Lolo Alexander alimchezea rafu mbaya Kazimoto na hakuweza kurudi uwanjani katika dakika ya 89. Stars ilishindwa kufanya mabadiliko kutokana na kumaliza wachezaji wake wote wa akiba

Katika mchezo huo Stars iliwakilishwa na: Kaseja, Kapombe, Maftah, Yondan, Agrey Morris, Shaaban Nditi, Salum Aboubakar/John Boko, Frank Domayo, Mbwana Samatta, Ngassa na Mwinyi Kazimoto.

Ivory Coast: Bary Boubacar, Emmanuel Eboue, Tiene Siaka, Kolo Toure, Lolo Igor, Gosso Gosso Jean, Yao Kouassi, Cheikh Tiote, Didier Drogba na Solomon Kalou.