![]() |
Arthur Wharton |
Shirikisho la Soka la Kimataifa, Fifa, limemtunuku Tuzo ya Mwanasoka wa Kwanza mwenye asili ya Afrika kucheza soka ya kulipwa, Arthur Wharton.
Fifa ilitoa tuzo hiyo kwa mchezaji huyo aliyekuwa akiichezea Darlington ya England. Shughuli hiyo ya tuzo ilifanyika Makao Makuu ya Fifa mjini Zurich.
Rais wa Fifa, Sepp Blatter, alisema kuwa shirikisho lake limefanya hivyo kuonyesha kuwa hakuna ubaguzi wa rangi katika soka.
"Hii ni siku muhimu kwa Fifa," alisema.
"Tunafanya kazi kupinga ubaguzi. Soka inaunganisha watu, inaleta watu karibu, na tunamtunuku kupitia Arthur Wharton Foundation," alisema Blatter.
"Alikuwa mwanasoka wa kwanza mwenye asili ya Afrika kucheza Ligi Kuu England lakini tunajiuliza, imechukua muda gani hadi mchezaji mweusi kuitwa kwenye timu ya taifa ya England, ni kama miaka 100."
"Mwanasoka huyu tayari anafahamika Wembley na FA imechanga pauni 20,000 kama heshima yake Darlington katika mfuko wake wa maendeleo ya soka.
Wharton alikuwa raia wa Gold Coast (sasa Ghana), alikwenda England mwaka 1884, akiwa na miaka 19. Alikuwa na mpango wa kucheza soka katika klabu ya Methodist iliyoko Cleveland College, Darlington.
Mwaka 1886 alikuja kuwa mkimbiaji wa mita 100 na alishinda mbio hizo. Mwaka mmoja baadaye alishinda mbio za baiskeli zilizokuwa zikishindanwa kutoka Preston hadi Blackburn.
Uwezo wake katika michezo ulionwa na Klabu ya Darlington ambayo ilimsajili kama golikipa na aliidakia kuanzia 1885 hadi 1888 na kuwa Mwafrika wa kwanza kucheza soka ya kulipwa England. Alizichezea pia Preston North End, Stockport County na Sheffield United.
Mfanyabiashara na mmiliki wa Darlington FC, Shaun Campbell alimsajili Wharton kwa zaidi ya miaka mitano.
"Ni wazi kutambuliwa kwake na Fifa ni sehemu ya mafanikio na kunaupa nguvu mfuko wa Arthur Wharton," anasema Blatter.
No comments:
Post a Comment