Vijana wa Kim Poulsen timu ya soka ya Tanzania maarufu kama Taifa Stars imepigana kufa na kupona leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya timu ya Taifa ya Gambia.
Gambia ndio waliokuwa wa kwanza kufunga goli lililowekwa kimiani mnamo dak. 7 ya mchezo na Ceesay, Taifa Stars walijitajidi kadri ya uwezo wao kusawazisha bao hili lakini kosakosa nyingi langoni mwa Gambia hazikuzaa matunda hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.
Dakika ya 60 kipindi cha pili, Shomari Kapombe aliisawazishia Taifa stars kufuatia klosi nzuri iliyopigwa na Erasto nyoni ikitokea winga ya kulia.
Watanzania wakiwa na matumaini ya kupata ushindi walizidi kulisakama lango la Gambia mara baada ya kusawazisha goli lakini Wagambia hao walikuwa na safu nzuri ya ulinzi iliyowapa tabu sana vijana wa Tanzania.
Mnamo dakika ya 84 beki wa Gambia alinawa mpira kwenye eneo la hatari kufuatia klosi hatari iliyopigwa na Mbwana Samatta. Erasto Nyoni alipiga kwa ustadi mkubwa penati hiyo na kuiandikia Stars bao la 2 na la ushindi.
Mpaka sasa Stars inashika nafasi ya pili iliwa na pointi 3, pointi moja nyuma ya vinara Ivory Coast wenye pointi 4 baada ya kutoka sare hiyo jana na Morroco. Gambia wao wanashika mkia wakiwa na pointi 1 baada ya kutoa sare mchezo wao wa kwanza dhidi ya Morroco.
No comments:
Post a Comment