Pages

Monday, 4 June 2012

JOHN BARNES: FERDINAND HANA HAKI YA KUICHEZEA ENGLAND

Rio Ferdinand katika moja ya mechi na timu ya Taifa ya England
John Barnes na David Pleat wameunga mkono uamuzi wa kocha wa timu ya Taifa ya England Roy Hodgson wa kutomjumuisha kwenye kikosi chake mchezaji mkongwe wa Manchester United Rio Ferdinand.

Mapema week hii baada ya kocha Roy kuthibitisha kuwa beki wa kati wa Chelsea Gary Cahill hataweza kuiwakilisha nchi yake kwenye michuano ya Euro 2012 inayotarajiwa kuanza mapema mwezi huu, kocha huyo aliamua kumuita kwenye kikosi chake kinda Martin Kelly ilikuziba pengo la beki huyo.

Kitendo hicho kilionekana kuwakera baadhi ya wadau wa soka wanaomsupport beki wa Man United Rio Ferdinand.

Mwakilishi wa beki huyo [Jamie Moralee] amemtuhumu kocha Roy pamoja na shirikisho la soka nchini Uingereza kuwa limemkosea heshima mchezaji huyo kwa kutomjumuisha kwenye kikosi chake kitakachoshiriki michuano ya Euro 2012.

Lakini suala hili limechukua sura mpya baada ya David Pleat kushangazwa na kauli hiyo ya Moralee huku akiita kauli hiyo kuwa iko nje ya majukumu [out of order].

Naye John Barnes amesema "Soka la kimataifa la kila mmoja hufika kikomo, kumuacha mtu kwenye kikosi cha timu ya taifa si kumkosea heshima"

"nilicheza michezo 79 nikiwa na timu ya taifa na niliachwa nje ya kikosi kwa sababu muda wangu wa kuichezea timu ya taifa ulikuwa umekwisha. Suala lilibaki ni kumuunga mkono kocha" Barnes aliendelea kusema.

Rio amekwisha cheza michezo 81 na timu ya taifa ya England , aliachwa kwenye kikosi cha kwanza cha Roy kabla ya kuachwa tena baada ya Cahill kupatwa na majeraha yaliyomfanya kocha huyo kumuweka kando ya kikosi chake kitakachoshiriki micchuano ya Euro 2012.


No comments:

Post a Comment