KIKOSI BORA CHA LIGI KUU UINGEREZA 2011-2012
Ikielekea ukingoni ligi ambayo kwa muono wangu naona ndiyo ligi bora kuliko zote duniani, English Premier League, wachezaji wafuatao kutokana na performance zao walizoonyesha mpaka sasa ndiyo wanaounda kikosi cha msimu wa mwaka 2011-2012 wa ligi kuu England.
GOALKEEPER: JOE HART
Akiongoza kwa kuwa na clean sheet 13 mpaka sasa, goalkeeper kinda na mzawa wa England ndiye anayesimama kwenye milingoti mitatu kuunda kikosi bora kabisa cha English Premier League kwa msimu huu wa 2011-2012. Ni mtu tegemeo sana kwenye club yake ya Manchester City pamoja na timu ya Taifa ya England.
RIGHT-BACK: KYLE WALKER
Kinda mwenye umri wa miaka 21 amekuwa moja ya nguzo na mhimili mkuu wa safu ya ulinzi ya Tottenham kwa msimu huu, akicheza mechi 38 katika mashindano yote mpaka sasa msimu huu Walker ameonekana kama nyota inayotarajiwa kufanya makubwa zaidi pale white hart lane.
CENTRE-BACKS: VICENT COMPANY & THOMAS VERMAELEN
Wawili hawa wakikaa pamoja watatengeneza moja kati ya defence ngumu na tishio kwa mshambuliaji wa aina yoyote ile duniani. Company amekuwa moja kati ya nguzo muhimu sana katika safu ya ulinzi wa City msimu huu, akiwa kama kiongozi ameonyesha nini kinatakiwa kufanyika ili timu ipate ushindi pia isifungwe magoli na wapinzani.
Arsenal wakifungwa jumla ya magoli 6 katika mechi zao 11 za mwisho, ''The Verminator'' kama mashabiki wa the gunners wanavyomwita amekuwa nguzo ya safu ya ulinzi ya Arsenal tangu alipopona majeraha yake mapema mwanzoni mwa msimu.
LEFT-BACK: LEIGHTON BAINES
Guu la kushoto la limekuwa ndiyo silaha kubwa kwenye mipira iliyokufa kiasi cha kuisaidia Everton kufikia hapa ilipo leo, Baines amekuwa akija kwa kasi sana tangu msimu ulioisha wa mwaka 2010-2011 kiasi cha kutishia namba ya Ashley Cole kwenye timu ya taifa ya England.
MIDFIELD: DAVID SILVA, YAYA TOURE, SCOTT PARKER & GALETH BALE
Wkicheza mtindo wa 4-4-2 hawa jamaa ndiyo viungo bora kabisa kwa msimu huu katika EPL, David Silva akicheza mechi 29 msimu huu mpaka sasa Silva ndo mchezaji anayeongoza kwa kuwa na assist nyingi kuliko mchezaji yoyote yule msimu huu sawa na Antonio Valencia wa Man United Juan Mata wa Chelsea....akicheza assist 13 zilizoisadia City kuwa kileleni mwa league kwa tofauti ya magoli.
Yaya Toure na Scott Parker wakikaa pamoja kwenye dimba watatengeneza moja kati ya kiungo kigumu kupitika, wote wamedhihilisha hayo kwenye vilabu vyao. Naye Galeth Bale kwa kasi aliyonayo amekuwa moja kati ya wachezaji wanoleta shida kwenye ngome ya ulinzi ya timu pinzani, the Welish International ni moja kati ya wachezaji wanaowaniwa na vilabu vikubwa baraani ulaya kutoka na kiwango chake.
ATTACK: WAYNE ROONEY & ROBIN VAN PERSIE
Wakifunga jumla ya magoli 54 wote kwa ujumla mpaka sasa katika msimu huu, Wayne Rooney akicheza kwa kiwango cha juu kwa misimu kadhaa sasa akiwa na United amekuwa tegemeo kuu la safu ya ushambuliaji la Sir Alex. Naye Van Persie kwa juhudi zake binafsi ameweza kuifikisha Arsenal kwenye matumaini ya kumaliza kwenye nafasi nzuri ya kushiriki Champions League msimu ujao kwani ndiye mchezaji aliyefunga magoli mengi na mhimu kwa Arsenal msimu huu.
kwa hakika timu yoyote ile Duniani ikikutana na kikosi hiki itakuwa na wakati mgumu sana kuweza kupata ushindi kutokana ka kikosi tajwa hapo juu kusheheni wachezaji wenye skills za ajabu na uwezo binafsi wa kuisaidia timu kupata ushindi.
No comments:
Post a Comment