Washika bunduki wa Kusini mwa London Arsenal Football Club wamefanikiwa kunasa sahihi ya mshambuliaji mahili wa Ujerumani na timu ya Fc Cologne baada ya kuisaka kwa muda mrefu kuanzia mwishoni mwa mwaka jana. Podolski (26) atajiunga rasmi na Arsenal mara baada ya kumalizika kwa ligi kuu msimu huu.
Akieleza mara baada ya uhamisho kukamilika, Lucas amesema ni furaha kupata nafasi kubwa na muhimu maishani mwake kwa kucheza Arsenal kwani kutamsaidia kuongeza kipaji chake........."haukuwa uamuzi rahisi sana kufanya kwangu, Cologne ni timu iliyomoyoni mwangu na itaendelea hivyo daima, kwa sasa tunahitaji kuwa makini ili kuisadia timu isishuke daraja.
Nina furaha sana kujiunga na Arsenal na pia kucheza EPL, Arsenal ni timu kubwa Ulaya na yenye historia style yao ya uchezaji ni nzuri na pia ina wachezaji wenye viwango vya hali ya juu sana, nasubiri kwa hamu sana kucheza mechi yangu ya kwanza pale Emirates Stadium."
Podolski alimaliza kwa kusema uamuzi aliofanya si kwamba anaichukia Cologne bali ni kwa maendeleo yake binafsi kwenye mpira.
Naye Mwenyekiti wa Fc Cologne Claus Horstmann amesema Cologne inamasikitiko makubwa kumpoteza mchezaji muhimu mwenye kipaji cha kipekee.....Lucas ni mchezaji wa hadhi ya juu duniani na mwenye mahusiano mazuri na mashabiki wa Fc Cologne pamoja na jiji lake na ndio maana tunasikitika sana kuondokewa na mchezaji kama yeye.
Huku mwenyekitiki wa Cologne akisikitika kocha wa Arsenal Fc Arsene Wenger anafuraha kubwa kukamilisha usajili wa Podolski kwa dau linalokaririwa kufikia paundi za kiingereza milioni 11
No comments:
Post a Comment