Pages

Tuesday, 8 May 2012

HAZARD: NITAVAA JEZI YA BLUE MSIMU UJAO

Eden Hazard
Baada ya kuhusishwa na Premier League kwa muda mrefu na yeye mwenye kuthibitisha kuwa atacheza ligi hiyo maarufu duniani msimu ujao, mchezaji mahiri wa timu ya Lille inayoshiriki ligi kuu nchini France amenukuliwa na vyombo vya habari akisema "nitavaa jezi ya blue msimu ujao"

Tetesi za mwanzo zikimhusisha kutua Arsenal, M-Belgiji huyu amekiri wazi kuvutiwa na ligi kuu nchini Uingereza na kuweka wazi kuwa atavaa uzi wa blue. 
Timu za Chelsea na Manchester City zimekuwa zikihusishwa hivi karibuni kuwania sahihi ya mchezaji huyo, Kocha wa Manchester United pia aliwahi kukiri mapema mwaka huu kuvutiwa na kijana huyo toka Belgium.

Eden Hazard aliamsha ari ya vilabu vya soka nchini Uingereza kusaka kwa udi na uvumba sahihi yake baada ya kuweka wazi nia yake ya kucheza nchini England baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya PSG mwezi uliopita.

Watabiri wengi wanamhusisha Hazard kutua Etihad Stadium hususani baada ya mchezaji huyo kusafiri toka Ufaransa kuja kushuhudia mchezo kati ya Manchester City na Manchester United mwishoni mwa mwezi April.

Hilo likadhidi kuthibitika baada ya yeye mwenyewe kuulizwa kuwa ni jezi gani kati ya nyekundu/red na blue angependa kuvaa msimu ujao, jibu lake likawa ni blue.

No comments:

Post a Comment