Habari zilizo zagaa kwenye vyombo vya habari duniani ni kuwa Arsenal imefikia makubaliano na club ya Rennes juu ya usajiri wa kiungo mkabaji Yann M'Vila.
Dau linaloaminika kufikia pound za kiingereza mil. 17.7, ikiwa Arsenal watafanikiwa kumnyakua kiungo huyo wa kifaransa kwa dau hilo basi itakuwa ni rekodi kwa Arsenal kusajili mchezaji kwa dau kubwa kama hilo. Mchezaji pekee aliyewahi kusajiliwa kwa dau kubwa na Arsene Wenger ni Andre Arshavin mwaka 2009 kwa dau la paundi mil 15 za kiingereza.
Beki wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa na Chelsea Marcel Desailly ameuambia mtandao wa goal.com kuwa M'Vila ni zaidi ya Patrick Vieira aliyecheza Arsenal kwa miaka 9 na kusisitiza zaidi kuwa kama angekuwa Mwenyekiti wa timu yoyote ile nchini Uingereza basi angefanya juu chini kuweza kumsainisha kiungo huyo mwenye miaka 21 toka Ufaransa.
Akijaribu kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao, Wenger tayari amekwisha nasa sahihi ya mshambuliaji toka club ya Cologne Lukas Podolski. Pia Wenger anafanya hivyo ilikumshawishi Van Persie asaini mkataba mpya baada ya ule alionao kuelekea ukingoni.
Yann M'Vila amecheza michezo 36 akiwa na Rennes msimu huu, huku timu yake hiyo ikiwa nafasi ya 6 kwenye msimamo wwa ligi kuu nchini Ufaransa, pia ataiwakilisha France kwenye michuano ya Euro 2012.
No comments:
Post a Comment