Pages

Monday, 7 May 2012

JINSI TIMU ZA MANCHESTER ZILIVYOANZA MBIO ZA KUSAKA UBINGWA WA ENGLISH PREMIER LEAGUE

Huu umekuwa moja ya msimu unaovutia sana katika historia ya English Premier League, timu mbili kutoka kwenye jiji la Manchester zikiwa na nafasi kubwa ya kuchukua kombe la ligi msimu huu. Swali la kujiuliza, Je, ni kwa jinsi gani timu hizi zilianza kampeni ya kusaka ubingwa msimu huu?


Msimu huu wa 2011-2012 wa Premier League ukielekea ukingoni huku timu zote kutoka jiji la Manchester zikiwa na pointi 86 huku Manchester City wakiongoza ligi kwa tofauti ya magoli 8. Kwa mujibu wa John Stammers mchambuzi wa Goal.com amejaribu kuangalia mbio hizi za ubingwa mwezi hadi mwezi tangu ligi hii ilivyoanza mwezi wa nane mwaka jana.
ROUND YA KWANZA - MWEZI WA NANE


Kabla ya ligi kuanza kwa msimu katika ya mwaka jana Man United walikuwa na nafasi kubwa ya kuchukua kombe hili, wakitokea nyuma kwa magoli mawili katika ushindi wa ngao ya hisani pale Wimbley United walionyesha dhahiri wanayo nia ya kutetea taji lao msimu huu.

Msimu ulipoaanza timu zote zilianza vizuri, Man City wakiwafundisha nidhamu vijana wageni kwenye Premier timu ya Swansea City United wao walisubiri goli la kujifunga dakika za mwisho ili kusahihisha makosa ya David De Gea dhidi ya West Brom. Magoli 4 ya Dzeko dhidi ya Spurs yaliipeleka City kileleni, hata hivyo United walijibu mapigo na kurudi kileleni baada ya kuisambaratisha Arsenal kwa jumla ya magoli 8-2 na kurudi tena kileleni. Mwanzoni mwa msimu uliwaona vijana wa Sir Alex wakiwa kileleni.

JUDGES' SCORECARDS
JUDGE 1: BARRY REDHAT..JUDGE 2: BENNY DOGLEASH.JUDGE 3: MONSIEUR WINGER

VERDICT: MANCHESTER UNITED'S ROUND


ROUND YA PILI - SEPTEMBER

Magoli yaliendelea kutililika kwa vijana wa jiji la Manchester kwa Kun Aguero kuifungia City magoli 3 dhidi ya Wigan, United walijibu mapigo kwa kuichabanga Bolton magoli 5-0 huku Rooney akifunga hat-trick nyingine baada ya kufunga dhidi ya Arsenal.

Week iliyofuata City walipoteza pointi mbili baada ya kutoka sare kwenye uwanja wa Craven Cottage baada ya kuwa mbele kwa magoli 2-0, Ilikuwa ni faida kwa United kuongoza ligi baada ya kuifunga Chelsea. Hata hivyo mechi iliyofuata United walipoteza pointi dhidi ya Stoke City huku Man City wakishinda dhidi ya Everton, hata hivyo round hii pia iliisha kwa United kuongoza ligi kwa tofauti ya magoli.

JUDGES' SCORECARDS
JUDGE 1: BARRY REDHAT..JUDGE 2: BENNY DOGLEASH.JUDGE 3: MONSIEUR WINGER

VERDICT: MANCHESTER UNITED'S ROUND


ROUND YA TATU - OCTOBER


City walianza na mkosi mwezi huu baada ya mchezaji wa zamani ya United Carlos Tevez kugoma kufanya mazoezi mepesi (warm up) kwenye mchezo wa UEFA Champions League dhidi ya Bayern Munich. Hata hivyo hilo halikuathiri sana kwani City walishinda mchezo wao ugenini dhidi ya Blackburn Rovers, United wakajibu mapigo kwa kuifunga Norwich City.

Baada ya hapo kasi ya kukimbizani kileleni ikazidi kushika kasi, hii ilitokea baada ya Man City kuisambalatisha United pale Old Traford kwa magoli 6-1 huku ikiaminika kuwa hiki ndicho kipigo kikubwa kwa Sir Alex kukipata katika maisha yake akiwa kama kocha. City wakageuza ubao na kuongoza ligi.

JUDGES' SCORECARDS
JUDGE 1: BARRY REDHAT..JUDGE 2: BENNY DOGLEASH.JUDGE 3: MONSIEUR WINGER

VERDICT: MANCHESTER CITY'S ROUND


ROUND YA NNE - NOVEMBA

Man City waliendelea na rekodi yao ya kutopoteza mchezo baada ya ushindi mwembamba dhidi ya QPR, goli pekee la Mhispania aliyeonekana kuwa kwenye kiwango cha hatari ( David Silva) waliwasaidia City kubaki kileleni. United wakionyesha kiwango cha kawaida sana, walitegemea goli la kujifunga toka kwa beki wao za zamani Wes Brown ili kuishinda Sunderland, baadae tena walipata shida kuvunja rekodi ya Swansea City ya  kutopoteza mchezo nyumbani baada ya kuifunga kwa tabu.

Magoli na ushindi viliendelea kutiririka kwa City baada ya kuifunga Newcastle, hata hivyo mambo hayakuwa mazuri sana kwa Balloteli baada ya kutolewa nje kwa kadi mbili za njano kwenye mchezo dhidi ya Liverpool, City wakitoa droo ya 1-1. Hata hivyo vijana wa Manchin waliendelea kuongoza ligi baada ya United kutoa droo na Newcastle. Mwezi ukaisha kwa City wakiongoza kwa tofauti ya pointi 5.

JUDGES' SCORECARDS
JUDGE 1: BARRY REDHAT..JUDGE 2: BENNY DOGLEASH.JUDGE 3: MONSIEUR WINGER

VERDICT: MANCHESTER CITY'S ROUND


ROUND YA TANO - DECEMBA

Mwezi decemba ukaanza vizuri kwa City, magoli mawili ya Aguero na Balloteli yaliipatia City ushindi dhidi ya Norwich City huku mabingwa watetezi wakiendelea kusuasua baada ya ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Aston Villa. Siku chache baadae timu zote toka jiji la Mancherster zikapata pigo baada ya kutolewa kwenye michuano ya Klabu Bingwa barani ulaya kwenye hatua ya makundi.

Pia mwezi huu ulishuhudia City wakipoteza mchezo wao wa kwanza kwenye EPL baada ya kufungwa na Chelsea goli 2-1, hii  ikawa faida kwa United baada ya kushinda goli 4-0 dhidi ya Wolves na kupunguza tofauti ya pointi kuwa 2. 

Week chache baadae Red devils walizinduka na kupata ushindi dhidi ya QPR, FULHAM na WIGAN, huku City baada ya ushindi mwembamba wa goli 1-0 dhidi ya Arsenal wakatoa droo ya bila kufungana na West Brom siku ya Boxing day.

Mwaka mpya ukaanza vibaya kwa United baada ya kupokea kipigo nyumbani cha magoli 3-2 dhidi ya Blackburn, makosa ya De Gea yakiigharimu timu. Round hii ikaisha kwa United kwenda sawa na City kwenye msimamo wa ligi.
JUDGES' SCORECARDS
JUDGE 1: BARRY REDHAT..JUDGE 2: BENNY DOGLEASH.JUDGE 3: MONSIEUR WINGER

VERDICT: MANCHESTER UNITED'S ROUND



ROUND YA SITA - JANUARY

City wakapoteza nafasi ya kuizidi pointi United baada ya kupokea kipigo cha goli 1-0 toka kwa Sunderland, hata hivyo wakazinduka mechi iliyofuata kwa kuitandika Liverpool 3-0 huku United wakipokea kipigo cha 3-0 toka kwa Newcastle.

Round hii ya sita ikaona ujio wa kiungo mahiri wa United Paul Scholes kuongeza nguvu kwenye kikosi kilichokosa mbadala wake tangu alipostaafu na pia kutokana na United kuandamwa na majeruhi. Alicheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya City kwenye FA CUP huku Yaya Toure mchezaji mhimu kwa City akikosekana baada ya kuwa kwenye majukumu ya Kitaifa kwenye AFCON 2012. Makosa ya De Gea yakazidi kuigharimu tena United kwenye mchozo wa FA CUP dhidi ya Liverpool.

Ujio wa Scholes ulionyesha kuwa na umuhimu mkubwa kwa United baada ya kushinda mechi tatu mfululizo dhidi ya Bolton , Arsenal, na Stoke City. Hali haikuwa nzuri kwa City baada ya kuwakosa wachezaji wake wa kiafrica kwani waliweza kushinda michezo 2 dhidi ya Wigan na Tottenham, na kupoteza ule wa Everton. Hata hivyo city wakamaliza round hii wakiwa juu ya United.

JUDGES' SCORECARDS
JUDGE 1: BARRY REDHAT..JUDGE 2: BENNY DOGLEASH.JUDGE 3: MONSIEUR WINGER

VERDICT: MANCHESTER CITY'S ROUND



ROUND YA SABA - FEBRUARY

Kwenye raundi hii ya saba vijana wa Manchini wakihangaika kurudisha kiwango chao walichoanza nacho mwanzoni mwa msimu, City wakaifunga Fulham 3-0 huku United wakitoka sare ya 3-3 na Chelsea kwenye moja kati ya michezo ya kuvutia msimu huu. Baadae United wakaifunga Liverpool pale Old Traford kwenye mchezo uliomalizika kwa utata kati ya Luis Suarez huku City wakishinda Villa Park baada ya ujio wa akina Toure.

Timu zote zikishinda michezo yao ya mwisho wa mwezi huku De Gea akionyesha kubadilika sana kwa kiwango chake kuanza kukaa sawa, City walimalimaliza roundi hii kwa tofauti ya pointi 2.

JUDGES' SCORECARDS
JUDGE 1: BARRY REDHAT..JUDGE 2: BENNY DOGLEASH.JUDGE 3: MONSIEUR WINGER

VERDICT: MANCHESTER CITY'S ROUND



ROUND YA NANE - MARCH

Baada ya timu zote za Mancherster kushinda michezo yao ya mwanzo mwa raundi hii, United wakapindua ubao wa msimamo wa ligi baada ya kushinda 2-0 dhidi ya West Brom huku City akipokea kipigo  cha 1-0 toka kwa Swansea City. Waliendelea kushinda mechi zao dhidi ya Wolves huku ujio wa Scholes ukidhihirisha kuwa ulikuwa ni wa muhimu kwa United.

Kushuka kwa kiwango kwa David Silva na Dzeko kukapelekea kocha wa City kumrudisha kwenye kikosi cha kwanza Carlos Tevez baada ya kuwa nje tangu mwezi October baada ya kutofautiana na kocha wake, ujio wa Tevez ukaisaidia City kupata ushindi dhidi ya Chelsea.

Hata hivyo vijana wa Manchini walimaliza roundi hii vibaya baada ya kutoa sare na Stoke na Sunderland na kuwa nyuma ya United kwa pointi 2.
JUDGES' SCORECARDS
JUDGE 1: BARRY REDHAT..JUDGE 2: BENNY DOGLEASH.JUDGE 3: MONSIEUR WINGER

VERDICT: MANCHESTER UNITED'S ROUND


ROUND YA TISA - APRIL

United wakaendeleza ushindi walioupata mwezi wa tatu mwanzu mwa mwezi wa nne baada ya ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Blackburn na QPR huku mpinzani wa zamani wa Sir Alex, Arsene Wenger akiisaidia United kwa kuifunga City 1-0. 

Hali ikageuka tena kwa United baada ya kupokea kipigo toka kwa Wigan, huku Tevez akirudi kwa kishindi kwenye ushindi  dhidi ya West Brom huku akifanya hivyo tena kwenye ushindi mwingine wa 4-0 dhidi ya Aston Villa. City walionyesha kutokata tamaa baada ya kuifunga Norwich City 6-1 week chache baadae.

Man United walizidi kurusu City kuwasogelea zaidi baada ya kuruhusu sare ya 4-4 dhidi ya Everton United ikiingoza 4-2 hadi dakika ya 85 ya mchezo. 

Siku ya siku ikafika, mchezo wa mahasimu hao siku ya April 30 ukapigwa. City akienda kwenye mchezo huo akiwa nyuma kwa pointi 3, aliitandika United kwa goli 1-0 shukrani za dhati ziende kwa Vicent Kompany aliyefunga goli pekee la City kufuatia kona iliyopigwa na Silva.

Round ikaisha kwa City kurudi kileleni kwa tofauti ya magoli.



JUDGES' SCORECARDS
JUDGE 1: BARRY REDHAT..JUDGE 2: BENNY DOGLEASH.JUDGE 3: MONSIEUR WINGER

VERDICT: MANCHESTER CITY'S ROUND



ROUNDI YA KUMI - MAY

Zikiwa zimesalia mechi mbili ligi kumalizika, City akiwa kileleni kwa tofauti ya magoli. Akaifunga Newcastle 2-0 kwenye uwanja wa Sports Direct Arena magoli yote yakifungwa na Yaya Toure. Hata hivyo hiyo haikuwakatisha tamaa United kuendelea kupigana hadi dakika za mwisho baada ya kuifunga Swansea City kwa magoli 2-0.

Man United wakielekea kwenye mchezo wao wa mwisho dhidi ya Sunderland, huku wakiiombea njaa Man City itakayocheza mchezo wake wa mwisho Etihad Stadium dhidi ya QPR, City wameshinda wamepoteza mchezo mmoja tu kwenye uwanja wao huo. Kwa upande mwingine QPR watategemea miujiza kutokana na kuwa na record mbaya ugenini msimu huu.

Timu zote kuelekea mechi zao za mwisho zinatakiwa kuwa makini ili kuhakikisha hazipotezi michezo hiyo.


JUDGES' SCORECARDS
JUDGE 1: BARRY REDHAT..JUDGE 2: BENNY DOGLEASH.JUDGE 3: MONSIEUR WINGER

VERDICT: MANCHESTER CITY'S ROUND



















No comments:

Post a Comment