Manuel Almunia ni miongoni mwa wachezaji 7 walioambiwa na Arsenal kuwa watakuwa huru pindi mikataba yao itakapomalizika mwezi ujao tarehe 30 june.
Kipa huyo wa Kihispania aliyecheza kwenye fainali ya Champions league mwaka 2006 dhidi ya Barcelona ameshindwa kuonyesha cheche zake msimu huu wa 2011-2012 uliomalizika karibuni.
Almunia (35), alicheza kwa dakika 70 kwenye fainali hiyo ya UCL baada ya Jens Lehman kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumuangusha Eto'o.
Tangu ajiunge na Arsenal akitokea Celta Vigo july 2004, Almunia amecheza michezo 175 akiwa na gunners na kuweka cleen sheet 70. Manuel alitumia muda wake mwingi wa msimu akiwa kwa mkopo West Ham United baada ya Manager wa timu hiyo Sam Allardyce kugundua kuwa kipa wake Robert Green ana majeraha.
Beki Gavin Hoyte aliyecheza mchezo mmoja akiwa na kikosi cha kwanza ni miongoni mwa wachezaji watakao kuwa huru kuanzia june 30 mwaka huu. Wachezaji wengine ni; George Brislen-Hall, Sean McDermott, Rhys Murphy, James Campbell na Jeffrey Monakana.
Walaka uliotolewa kwenye mtandao wa klabu ya Arsenal umewashukuru wachezaji hao kwa mchango wao waliotoa tangu wajiunge na timu hiyo.
No comments:
Post a Comment