Pages

Wednesday, 23 May 2012

AZAM FC KWA MARA YA KWANZA NDANI YA KAGAME CUP

kikosi cha Azam
Timu ya soka ya Azam Fc yenye makazi yake Mbagala- Chamazi jijini Dar es Salaam ni miongoni mwa timu tatu zitakazo shiriki michuano ya Kagame itakayofanyika baadae mwaka huu. Hii itakuwa mara ya kwanza kwa timu hii kushiriki michuano hii inayoendeshwa na chama cha soka Afrika mashariki na kati CECAFA.

Wakati Azam wakishiriki kwenye michuano hii kwa mara ya kwanza huku ikiwa imemaliza ligi kuu Tanzania Bara ikiwa nafasi ya pili, Simba Sc wao watashiriki kama mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara huku timu ya vijana kutoka mitaa ya msimbazi, timu ya Yanga wao watashiriki michuano hii wakiwa kama mabingwa watetezi.

kwa habari zaidi kuhusu michuano hii endelea kutembelea blog hii:

No comments:

Post a Comment