![]() |
Drogba akishangilia ushindi wa UCL na Torres |
Mshambuliaji nguli wa Ivory Coast, Didier Drogba amewaambia wachezaji wenzake kwamba, anaondoka Chelsea kwa sababu hayuko tayari kutumia muda mwingi kama mchezaji wa akiba hapo, lilimkariri Jarida la France Football juzi Jumatatu.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 34, aliyefunga bao la kusawazisha na penalti ya ushindi dhidi ya Bayern Munich na kuiongoza Chelsea kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Jumamosi iliyopita, alikaririwa na jarida hilo kuwa alitokwa na machozi wakati alipowaambia wachezaji wenzake kwenye basi Jumapili walipokuwa wakitembeza kombe lao mitaani.
"Hatutakuwa pamoja msimu ujao," jarida hilo lilimkariri Drogba akisema.
"Kama nilivyoamua kuondoa, nilitaka kuwambia wote tukiwa tunatazama.
"Hicho ndiyo kitu pekee nilichoshindwa kufanya. Walinifanya nishindwe kuzungumza. Japokuwa nilishasema nitakuwa hapa kwa miaka mitatu, lakini sasa nataka kuondoka, napatwa na wakati mgumu kusema mwisho wangu umefika hapa.
" Nimechukua uamuzi huu mgumu kwa makusudi. Sitakuwa tayari kukaa benchi na kuangalia wengine wakicheza katika kipindi hiki ambacho klabu hii inataka kutegeneza timu mpya.
"Kwa hiyo muda umefika kwangu kuondoka, nitakwenda sehemu nyingine isiyojulikana.
"Nataka kutegeneza historia nyingine," aliongeza Drogba, ambaye maktaba wake umekwisha baada ya kuitumikia klabu hiyo tangu 2004 alipojiunga Chelsea akitokea Marseille.
Vyombo vya habari vya England vimedai nyota huyo wa Ivory Coast ana mpango wa kwenda kucheza soka China katika klabu ya Shanghai Shenhua, pamoja na rafiki yake Nicolas Anelka ambaye ni kocha mchezaji wa timu hiyo.
No comments:
Post a Comment