Pages

Tuesday, 8 May 2012

BAADA YA KUSHUKA DARAJA, BARUA KWENDA KWA MMILIKI WA BLACKBURN ROVERS YAVUJA

Steve akishindwa kuamini kama ndo kaiaga Premier League
Masaa machache baada ya timu ya Blackburn Rovers kushuka daraja rasmi huku ikiwa imebakiza mchezo mmoja msimu huu baada ya kipigo cha 1-0 ilichopata usiku wa jana toka kwa Wigan, barua ya ushauri toka kwa Deputy Chief Executive wa timu hiyo kwenda kwa owner wa timu hiyo imevuja rasmi saa chache baada ya timu hiyo kushuka daraja.

Barua iliyothibitishwa na Bw. Paul Hunt (Deputy Chief Executive) iliandikwa mwezi wa decemba mwaka jana baada ya Hunt kuona mwelekeo wa Blackburn kushuka daraja uko nje nje kama kazi ya ziada isipofanyika.

Barua hiyo iliyochapishwa kwenye mtandao wa Sportingintelligence.com umemnukuu Hunt akimuomba Bw. Venky ambaye ndiye mmiliki wa timu hiyo kufanya uwekezaji wa maana ili kuinusuru timu hiyo isishuke daraja, hususani kuhusu uongozi mzima na suala zima linalomhusu Kean ili kuiepusha timu isishuke daraja.

Pia barua hiyo imemnukuu Hunt akisema "...nimewahi kuombwa kumsupport Kocha na nilifanya hivyo kwa sababu nampenda Steve, nimemuunga mkono tangu mwanzo na nimekuwa nikiomba mema ili azidi kufanya vizuri.."

Lakini kwa sasa hari ni tofauti kabisa, nadhani muda umefika wa yeye kuondoka kwani mashabiki wamekuwa hawamuungi mkono hata kidogo vivyo hivyo wachezaji nao hawataki kucheza chini yake hususani baada ya kupoteza mchezo wa jana dhidi ya Wigan. Alimalizia kusema Bw. Hunt

Hunt pia alimweleza mmiliki wa Blackburn kitendo cha mashabiki kuisusia timu, na kuzidi kumshauri kufanya mabadiliko yenye manufaa kwa club.

Kutokusikia kwa mmiliki huyo kunamfanya kumalizia mechi yake ya mwisho kwenye EPL na kurudi chini kushuhudia Blackburn ikicheza Championships.

No comments:

Post a Comment