![]() |
Toure Yaya |
Kiungo wa kimataifa wa Ivory Cost na timu ya Manchester City Yaya Toure ameelezea nia yake ya kumalizia maisha yake ya soka nchini hispania hususani Barcelona.
Toure (28) aliyecheza Barcelona kwa miaka mitatu, alijiunga na Manchester City mwaka 2010 kwa dau la pound 24 mil. za kiingereza. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast amedhihirisha umuhimu wake kwenye kikosi cha Manchin hasa baada ya kuiongoza City kwenye ushindi dhidi ya Newcastle.
Licha ya City kuwa na asilimia kubwa ya kushinda taji la ligi kuu England msimu huu, kiungo huyo hajasita kueleza nia yake ya kurejea Camp Nuo. Akieleza kwenye mkutano na waandishi wa habari ansema "....miaka miwili iliyopita nilisema kuwa nitarejea, imekuwa ni timu muhimu sana maisha mwangu na kama ikitokea wakakuhitaji basi haina haja ya kufikiri mara mbili. Naipenda Barcelona...."
Yaya Toure ameitabilia Barcelona kufanya vizuri chini ya kocha mpya Tito Vilanova.
No comments:
Post a Comment