![]() |
mashabiki wa Blackburn wakiandamana |
Habari zilizoenea kwenye vyombo vya habari nchin Uingereza vinaeleza kuwa timu ya Blackburn Rovers imemtimua aliyekuwa Deputy Chief Executive Paul Hunt saa chache baada ya barua inayoaminika kuwa iliandikwa na Hunt mwenzi decemba mwaka jana kwenda kwa mmiliki wa timu hiyo kuvuja na kuchapishwa kwenye mtandao wa sportingintelligence.com.
Barua hiyo ilikuwa ikitoa ushauri kwa Venky ambaye ni mmiliki wa Rovers afanye mabadiliko ili kuisaidia timu isishuke daraja pia kusaidia kujenga uongozi imara.
Mapema hii leo sportingintelligence.com imechapisha taarifa kuwa Hunt amefukuzwa na Blackburn Rovers kufuatia taarifa za kuvuja kwa barua hiyo ingawa taarifa hazijamhusisha Hunt na kuvuja kwa barua hiyo.
Naye Kean akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari amesema kuwa amesikia tetesi hizo lakini hakuwa tayari kuzungumzia kwa wakati huo na kusisitiza anachofikiria ni mchezo dhidi ya Chelsea.
No comments:
Post a Comment