![]() |
Philipp Lahm |
Wakielekea kwenye fainali za UEFA CHAMPIONS LEAGUE mwezi huu, Captain wa timu ya Bayern Munich Philipp Lahm amesema timu yake ya sasa ni bora kuliko ile iliyocheza fainali za UCL msimu wa 2010.
The Bavarians waliopoteza mchezo wa fainali dhidi ya Inter Milan mwaka 2010, watacheza tena fainali hizo mwaka huu dhidi ya Chelsea kwenye uwanja wao uliopo Munich tarehe 19/05/2012. "Imani yetu ni kubwa kuliko miaka miwili iliyopita", Lahm aliwaeleza baadhi ya waandishi wachache waliokuwepo kwenye uwanja wa mazoezi wa Bayern siku ya alhamisi.
Alimaliza kwa kusema "sisi ni wachezaji bora katika umri wetu wa sasa"
No comments:
Post a Comment