![]() |
Sol Campbell |
Akicheza michezo 646 katika club tano tofauti katika historia ya maisha yake ya soka na michezo 73 kwa timu ya Taifa ya England. Sol alianza rasmi maisha yake ya soka la kulipwa akiwa na miaka 18 katika timu ya Tottenham Hotspur.
Tangu aanze soka mwaka 1992, Sol Campbell (37) amepata kuzichezea timu za Arsenal Fc, Nottingham Forest, Portsmouth, na Tottenham.
Sol Campbell alicheza kwa kwa miaka 10 akiwa na Spurs kabla ya kuhamia Arsenal uhamisho uliowapa hasira mashabiki wa Spurs, kuhamia Gunners ilikuwa ni neema kwake kwani alicheza kwa mafanikio makubwa pale Arsenal.
Campbell alikuwa moja kati ya kikosi cha "Invisible" kilichocheza msimu mzima wa English Premier League 2003-2004 bila kufungwa, akishinda vikombe 2 vya ligi kuu, viwili vya FA CUP akiwa na Arsenal Campbell ndo mchezaji aliyefunga goli la pekee la Gunners katika fainali ya UEFA Champions League mwaka 2006 Arsenal akifungwa 2-1 na Barcelona.
Pia mwaka 2008 akiwa kama Captain wa Portsmouth aliiongoza katika ushindi wa fainali ya FA CUP. Mchezo wake wa mwisho alicheza akiwa na Newcastle march 2011.
No comments:
Post a Comment