![]() |
Van Bommel |
Kiungo wa kimataifa wa Netherlands Mark Van Bommel (35) ataondoka AC Milan na kujiunga na timu yake ya zamani PSV Eindhoven mapema pindi dirisha la majira ya kiangazi litakapofunguliwa.
Van Bommel alijiunga na Milan akitokea Bayern Munich mwezi January mwaka 2011 amekuwa mchezaji wa nne kutangaza kuondoka Milan ndani ya week hii kufuatia Filippo Inzaghi, Gennaro Gattuso, na Alessandro Nesta kutangaza nia yao ya kuondoka klabuni hapo mapema week hii.
Akicheza PSV kuanzia mwaka 1999 - 2005 alipoondoka na kuhamia Barcelona, Van Bommel alishinda taji la ligi pamoja na Ligi ya Mabingwa barani Ulaya akiwa Camp Nuo.
AC Milan wameshindwa kutetea ubingwa wao baada ya kupokwa ubingwa huo na Juventus msimu huu.
No comments:
Post a Comment