![]() |
Vicenet del Bosque |
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uhispania Vicente del Bosque (61) ametangaza kikosi chake cha wachezaji 23 kitakachoiwakilisha Uhispania kwenye michuano ya Uefa Euro 2012 nchini Poland na Ukraine.
Kocha huyo wa kihispania amewaacha Adrian Lopez toka Atletico Madrid na Roberto Soldado toka Valencia huku akifanya mabadiliko ya wachezaji 9 baada ya kuwajumuisha kundini wachezaji toka Barcelona na Athletic Bilbao waliocheza fainali ya Copa del Rey siku ya Ijumaa.
Kuachwa kwa Adrian Lopez aliyeonyesha mchezo wa kuvutia kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Serbia pamoja na kuachwa kwa Soldado kumewashangaza wadau wengi wa soka nchini Spain na dunia kwa ujumla.
Mapema mwezi huu Vicente del Bosque alinukuliwa akisema kuwa Pedro atabaki nyumbani akitazama michuano hiyo kwenye luninga, hali imekuwa tofauti baada ya kocha huyo kumjumuisha mshambuliaji huyo toka Fc Barcelona hasa baada ya kufunga magoli mawili kwenye fainali ya Copa del Rey dhidi ya Bilbao.
Uhispania watatupa karata yao ya kwanza kwenye michuano hiyo ya Euro 2012 dhidi ya Italia (june 10) kabla ya kucheza na Jamhuri ya Ireland (june 14) na baadae Croatia (june 18)
Kabla ya kuanza kwa michuano hiyo, mabingwa hawa wa Dunia na Ulaya watacheza tena michezo yao ya kirafiki dhidi ya Korea Kusini na Uchina.
KIKOSI CHA UHISPANIA KUELEKEA UERO 2012
Jina | Klabu |
Makipa: | |
Iker Casillas | Real Madrid |
Pepe Reina | Liverpool |
Victor Valdes | Barcelona |
Mabeki: | |
Raul Albiol | Real Madrid |
Jordi Alba | Valencia |
Alvaro Arbeloa | Real Madrid |
Sergio Ramos | Real Madrid |
Juanfran Torres | Atletico Madrid |
Gerard Pique | Barcelona |
Javi Martinez | Athletic Bilbao |
Viungo/Midfielders: | |
Sergio Busquets | Barcelona |
Xavi | Barcelona |
Andres Iniesta | Barcelona |
Xabi Alonso | Real Madrid |
Santi Cazorla | Malaga |
Cesc Fabregas | Barcelona |
David Silva | Manchester City |
Jesus Navas | Sevilla |
Juan Mata | Chelsea |
Washambuliaji: | |
Pedro | Barcelona |
Alvaro Negredo | Sevilla |
Fernando Torres | Chelsea |
Fernando Llorente | Athletic Bilbao |
No comments:
Post a Comment