![]() |
Shehata akiwa kazini |
Mwenyekiti wa klabu hiyo Mamdouh Abbas alitangaza jana jumamosi kuwa Shehata bado ni kocha mkuu wa timu hiyo na hawawezi kumwachia aondoke.
"tumekataa ombi lake la kujiuzulu, ni kocha wetu na bado ataendelea kuwa na sisi, kilichotokea wiki iliyopita ilikuwa ni kutokuelewana kwa mambo fulani lakini kwa sasa hali ni shwari" Abbas aliiambia supersport.com
Habari zilizoenea kwenye vyombo vya habari nchini Misri wiki iliyopita zinaonyesha kuwa Shehata aliamua kujiuzulu baada ya bodi ya Zamalek kutokufanyia kazi maombi yake ya kuwachukulia hatua za kinidhamu wachezaji Ahmed Mido Hossam na Mahmoud Abd Al Razek "Shikabala"
Hata hivyo Bodi ya klabu hiyo imeamua kumtimua kwenye kikosi chake Mido na kumshukuru kwa mchango wake aliotoa kwa kipindi chote akiwa na Zamalek.
"hatumuhitaji Mido kwa sasa lakini tutamuhitaji badae siku atakapo stafu soka yake ili awe aje kuwa moja kati ya memba wa bodi ya Zamalek, tunaweza tukawa tumempoteza kama mchezaji lakini tunaamini hatutampoteza katika hali ya kibinadamu" Ibrahem Yousef ambaye ni memba wa bodi aliiambia pia supersport.com
Katika mwendelezo wa habari hii, bodi ya klabu hii pia imemtoa kwa mkopo Shikabala baada ya kutokea mtafaruku kati yake na kocha Shehata kwenye mchezo dhidi ya Maghreb Fes kwenye michuano ya klabu bingwa barani Afrika.
Zamalek itarudi tena kambini kuanzia tarehe mosi june mwaka huu.
No comments:
Post a Comment