Pages

Friday, 25 May 2012

FAMILIA YA ALEX OXLADE-CHAMBERLAIN KUTOSAFIRI KUSHUHUDIA MICHUANO YA EURO 2012

Chamberlain 
Familia ya kiuongo mahiri wa Arsena na timu ya Taifa ya England, Alex Oxlade-Chamberlain imethibitisha rasmi kuwa haitosafiri kuelekea nchini Ukraine na Poland kushuhudia michuano ya EUFA EURO 2012 kwa kuhofia vitendo vya ubaguzi wa rangi vilivyo tawala kwa mashabiki wa nchi hizo.

British Foreign Office imeionya nchi ya Ukraine juu ya watu watokao Asia, wale wenye asili ya Africa na watu binafsi watokao kwenye dini zenye kundi dogo la watu kuchukua tahadhari mapema.

Timu ya England iliyopangwa group D pamoja na wenyeji Ukraine itaweka kambi yake nchini Poland, hii ni kwa ajili ya kuwafanya wachezaji wa timu hiyo ya England wasisafiri pamoja na familia zao kuelekea fainali hizo za Euro mwaka huu.

Theo Walcott pia alithibitisha mapema mwezi huu kuwa familia yake haitosafiri kushuhudia michuano hiyo kwa kuhofia vitendo hivyo vya kibaguzi, huku habari zikizagaa Ijumaa hii kuwa Chamberlain (18) pia amefanya uamuzi kama huo.

Vitendo vya kibaguzi vinavyoendelea kutokea nchini Ukraine imekuwa hofu kwa baadhi ya wachezaji wa Timu ya England kusafiri na familia zao. Suala hili linabakia mikononi mwa UEFA kufanya juu chini ili kudhibiti hali hii isijitokeze kwenye michuano hii mikubwa duniani.

No comments:

Post a Comment