Pages

Thursday, 31 May 2012

BREAKING NEWS: ROGERS KOCHA MPYA WA LIVERPOOL

Brendan Rogers enzi zake akiwa Swansea City
Kocha aliyeifundisha timu ya Swansea City msimu uliokwisha mapema mwezi huu, Brendan Rogers atamridhi Kenny Dalglish kama kocha mkuu wa Liverpool kuanzia msimu ujao. Kocha huyo amechukua uamuzi huo baada ya kufanya mazungumzo na mmiliki wa klabu ya Liverpool na tajiri huyo kufikia makubaliano ya kimsingi na Swansea City kulipa fidia ya kumtoa Rogers Swansea.

kwa habari zaidi endelea kusoma blog hii.

Wednesday, 30 May 2012

WEMA SEPETU AVISHWA PETE NA MWINYI KUTOKA MACHOZI BAND @NEW MAISHA CLUB USIKU WA TAREHE 30 MAY

 Peter Moe & Gadna G Habash

 Mateja & Snura

 Sam Machozi, Snura & Sharo Millionaire

 Jamillar, Chaz Baba & Snura

 Abra & Choka wakipata shisha

 Wema Sepeta na Bodyguard wake

 Wema & Abou

 mmmmh....

 Jini Kabula

 Mtu mzima Mwinyi akaenda chini pwaaaa...

 Akakumbatiwa watu weweeeeeee

 Heeeh si akaweka pete kidoleni pale kabaaaaaaa

 Mabusu hihaaaaa, watu pipooooo

The End...

Picha zote na Dj Choka

Monday, 28 May 2012

ENGLAND YAPATA PIGO, GARETH BARRY APATA MAJERAHA

Barry akitoka nje baada ya kupata majeraha kwenye mchezo dhidi ya  Norway
Kiungo wa kimataifa wa England na Manchester City Gareth Barry ameondolewa kwenye kikosi cha wachezaji 23 cha England baada ya kupata majeraha ya kifundo cha mguu.

Kiungo huyo mwenye miaka 31 alifanyiwa uchunguzi mapema leo jumatatu kudhibitisha  majeraha hayo yaliyomlazimu kocha Roy Hodgson kumuacha nje ya kikosi chake mchezaji huyo wa kiungo cha kati.

"nina sikitika sana kumpoteza Gareth, ninaamini bado ananafasi kubwa ya kuichezea England baada ya michuano ya Euro" alisema kocha Roy Hodgson.

Hata hivyo kocha huyo amemuita beki wa timu ya Everton Phil Jagielka ili kuziba pengo la Barry kuelekea michuano hiyo mikubwa barani Ulaya.

Kifungu cha 17.05 cha Uefa kuelekea michuano hii ya Euro 2012 kinamruhusu kocha wa timu yoyote ile ya taifa kufanya mabadiliko ya mchezaji endapo itagundulika mchezaji husika amepatwa na majeraha makubwa yasiyoponyeka kwa wakati.

Kikosi cha mwisho cha England kuelekea michuano hii ya Euro kinatakiwa kuwasilishwa kwa UEFA katikati mwa siku ya jumanne.

CHELSEA WIN THE BATTLE TO SIGN HAZARD FROM LILLE


Belgian superstar has delivered a snub to Premier League champions Manchester City and their rivals Manchester United by opting to join the Stamford Bridge club

Eden Hazard is set to sign for Chelsea after finally making a decision on his future.

.The £32 million-rated Lille attacker is understood to have agreed personal terms with the Blues and is likely to sign for the Stamford Bridge club this week.

Manchester United and Manchester City were also given permission to talk to Hazard, but the 21-year-old decided over the weekend to sign for Chelsea, finally bringing the end to the ongoing transfer saga.

“It’s a done deal,” a source told Goal.com. “Hazard has made his choice and he will play for Chelsea next season.”
 HAZARD'S 2011-12 IN STATS
GAMES PLAYED
GOALS
ASSISTS
47
21
19
On Monday morning, the Belgian indicated that an announcement is imminent when he wrote on Twitter: "Good afternoon guys. I made up my mind. see you later. Thanks".

Chelsea are believed to have met the financial demands of Hazard and his agent, and also influenced his decision with the offer of a regular first team starting spot - something that would not have been a guarantee at City. 

The Blues stepped up their pursuit of one of Europe’s hottest talents following their triumph in the Champions League final, which guaranteed they will feature in Europe’s elite competition next season.

Hazard admitted after his final game for Lille that Chelsea’s astonishing triumph in Munich had forced him to reconsider his future, having previously been set on joining Roberto Mancini's Premier League champions.

“Chelsea could interest me now,” Hazard said. “They've won the Champions League and will therefore be in it next season. It's really important for me to be playing in that competition.

"Chelsea are a big club with some great players – of course it's a possibility.”

United and City had long been considered to be in a two-horse race for Hazard, but both clubs were believed to be concerned by the financial demands of the player's agent, who is understood to want £5 million for his part in any deal. 

Hazard was City’s primary close-season target - he attended the Manchester derby in late April as a guest of the club before being shown around houses in the area.

Chelsea's hijacking of the transfer, however, means Mancini has been dealt a chilling snub and Hazard is now set for a move to Chelsea, where Blues owner Roman Abramovich is ready to fund a regeneration of the squad over the summer.

The Ligue 1 player of the season is one of the most highly-rated talents in Europe and has been in stunning form, scoring 20 league goals and providing 22 assists.

MARK WEBBER AIBUKA MSHINDI MONACO


Mark Webber
Dereva kutoka Australia Webber 
Mark Webber aliibuka mshindi katika mashindano ya langalanga ya Monaco GP siku ya Jumapili, huu ukiwa ni ushindi wake wa pili huko katika kipindi chini ya miaka mitatu, na akiwatangulia madereva Nico Rosberg kutoka Ujerumani, na wa timu ya Mercedes, na Fernando Alonso kutoka Uhispania, na wa timu ya Ferrari.
Webber, dereva wa Red Bull, aliongoza mashindano hayo kutoka mwanzo hadi mwisho.
Dereva wa McLaren, Lewis Hamilton wa Uingereza, kuna wakati aliweza kujikita katika nafasi ya tatu, lakini akapitwa na dereva wa Ferrari Alonso, na vile vile Sebastian Vettel wa Red Bull, ambao walitumia mbinu bora za kuhakikisha walidumisha kasi yao na kumpita.
Wakati mmoja Alonso maksudi alibaki nyuma, ili kuokoa magurudumu yake, na ili yaweza kunasa barabara vyema katika dakika za mwishomwisho alipohitaji kasi kabla ya kuvifikia vituo vya kupata huduma ya gari kurekebishwa.
Mbinu hiyo hatimaye ilimsaidia kufanya vyema, kwani Webber na Hamilton waliposimama katika raundi ya 29, raundi mbili zaidi ya Rosberg, Alonso aliweza kwenda mzunguko mmoja zaidi, na akienda kwa kasi sana wakati huo.
Mbinu hiyo ilimwezesha kumtangulia Hamilton.
Dereva mwingine wa Uingereza, na wa timu ya McLaren, Jenson Button, alipata mashindano hayo kuwa magumu, na baada ya muda mfupi alilazimika kuondoka mapema.
Ushindi wa Mark Webber umeandikisha historia mpya katika mashindano ya Formula 1, kwa kuwa ni mara ya kwanza madereva sita tofauti kuibuka washindi baada ya mashindano sita ya msimu.
"Ninahisi nimefanikiwa kufanya maajabu," alielezea Webber kutoka Australia.”
"Ni siku ya ajabu kwa timu na mimi binafsi, na nimefurahi sana kupata tena ushindi hapa.”
Kufuatia matokeo hayo, Alonso wa timu ya Ferrari sasa anaongoza katika kuwania ubingwa wa dunia, akimtangulia Vettel na Webber kwa pointi tatu.
Hamilton anateremka kutoka nafasi ya tatu hadi nne, akiachwa nyuma na Alonso kwa pointi 13.

Sunday, 27 May 2012

YANGA KUWA CHINI YA SEKRETARIETI


Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikutana Mei 26 mwaka huu ili kutoa mwongozo wa nini kifanyike ndani ya Yanga baada ya wajumbe wake kudhaa kujiuzulu. Kamati ya Uchaguzi ya Yanga ilikuwa imeomba mwongozo huo TFF.
Baada ya kupata taarifa rasmi kutoka Yanga, Kamati imebaini kuwa Kamati ya Utendaji ya Yanga imekosa akidi baada ya wajumbe wake wengi kujiuzulu hivyo kutokuwa na uwezo wa kufanya uamuzi kwa mujibu wa Ibara ya 32(1) ya Katiba ya klabu hiyo.
Hivyo, Kamati imetoa mwongozo kwa Kamati ya Uchaguzi ya TFF ambayo ndiyo msimamizi wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga kuwa ili Kamati ya Utendaji ya Yanga iwe na nguvu za kikatiba kufanya shughuli zake ikiwemo uamuzi wa masuala mbalimbali ndani ya klabu hiyo ni lazima iwe na akidi.
Kwa mujibu wa Ibara ya 29(3) ya Katiba ya Yanga nafasi zilizo wazi katika Kamati ya Utendaji zinatakiwa kujazwa katika Mkutano Mkuu wa Kawaida ujao.
Pia Kamati imebaini uteuzi wa kujaza nafasi zilizo wazi za wajumbe uliofanywa na Kamati ya Utendaji ya Yanga, Mei 21 mwaka huu ni batili kwa vile Kamati ya Utendaji iliyofanya uteuzi huo haikuwa na akidi.
Ili kupata akidi na kufanya uamuzi Kamati ya Utendaji ya Yanga yenye wajumbe 13 inatakiwa kuwa na asilimia 50 ya wajumbe wote, hivyo ili wafanye uamuzi halali hawatakiwi kupungua saba.
Kwa wajumbe ambao hawajajiuzulu; Sarah Ramadhan, Mohamed Bhinda, Tito Osoro na Salim Rupia kwa sasa hawawezi kufanya shughuli zozote za Yanga hadi nafasi zilizo wazi katika Kamati ya Utendaji zitakapojazwa.
Kama inavyoelekeza Katiba ya Yanga, shughuli za kila siku za klabu hiyo zitaendelea kufanywa na Sekretarieti ya Yanga ambayo kiongozi wake ni Katibu Mkuu.
Alex Mgongolwa
Mwenyekiti
Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji 

TAIFA STARS, MALAWI ZAINGIZA MIL 40/-
Mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Malawi (The Flames) iliyochezwa Mei 26 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 40,980,000.
Mapato hayo yametokana na washabiki 10,767 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa viingilio vya sh. 3,000, sh. 5,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Washabiki 9,365 walikata tiketi za sh. 3,000.
 Asilimia 18 ya mapato hayo ambayo ni sh. 6,251,186 ilikwenda kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) wakati gharama kabla ya mgawo zilikuwa tiketi (sh. 4,999,800), waamuzi (sh. 1,105,000), usafi na ulinzi (sh. 2,350,000), maandalizi ya uwanja- pitch preparation (sh. 400,000), Wachina- Beijing Construction (sh. 2,000,000) na umeme (sh. 300,000).
Kwa upande wa mgawo asilimia 20 ya gharama za mechi ni sh. 4,714,803, asilimia 10 ya uwanja sh. 2,357,401, asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 1,178,701, asilimia 20 ya Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 4,714,803 na asilimia 45 ya TFF (sh. 10,608,306).

 TWIGA STARS UWANJANI ETHIOPIA LEO
Twiga Stars inacheza leo (Mei 27 mwaka huu) na Ethiopia katika mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) kuwania tiketi ya kucheza fainali zitakazofanyika Novemba mwaka huu nchini Equatorial Guinea.
Mechi hiyo itakayoanza saa 10 jioni kwa saa za nyumbani itafanyika kwenye Uwanja wa Taifa ulioko jijini Addis Ababa na timu hizo zitarudiana Juni 16 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 Kwa mujibu wa taarifa kutoka Addis Ababa, wachezaji wa Twiga Stars ambayo imefikia hoteli ya Churchil, leo saa 4 asubuhi wamefanya mkutano wa mwisho wa maandalizi ya mechi hiyo na kocha wao Charles Boniface Mkwasa na baadaye kupata chakula cha mchana kwa Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia.
 Twiga Stars; Fatuma Omari, Mwajuma Abdallah, Fatuma Bashiri, Fatuma Khatib, Evelyn Sekikubo, Mwapewa Mtumwa, Etoe Mlenzi, Mwanahamisi Omari, Ester Chabruma, Fatuma Mustafa na Asha Rashid.
Wachezaji wa akiba ni Maimuna Said, Semeni Abeid, Zena Khamis, Amina Ally, Rukia Hamis na Fadhila Hamad.
 Mchezo huo unachezeshwa na Angelique Tuyishime akisaidiwa na Sandrine Murangwa, Speciose Nyinawabari na Salma Mukansanga wote kutoka Rwanda. Kamishna ni Catherine Adipo kutoka Uganda.

 LIGI YA TAIFA KUANZA KUTIMUA VUMBI LEO
Ligi ya Taifa inayoshirikisha mabingwa wa mikoa inaanza kutimua vumbi leo kwenye vituo vya Kigoma, Musoma na Mtwara.
 Katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma, Flamingo ya Arusha inacheza na Forest ya Kilimanjaro (saa 8 mchana) wakati saa 10 jioni ni Ashanti United ya Ilala na Polisi ya Mara.
 Kituo cha Kigoma leo kina mechi moja tu kati ya Mwadui ya Shinyanga na JKT Kanembwa ya Kigoma itakayochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika kuanzia saa 10 kamili jioni.
 Tenende ya Mbeya na Kurugenzi ya Iringa ndizo zitakazoanza saa 8 mchana kwenye Kituo cha Mtwara na kufuatia na mechi kati ya Mpanda Stars ya Rukwa na Ndani ya Mtwara kuanzia saa 10 kamili jioni. Mechi hizo zinachezwa katika Uwanja wa Umoja.
 Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) 

SPAIN NAYO YAWEKA HADHARANI SILAHA ZA MAANGAMIZI KUELEKEA EURO 2012

Vicenet del Bosque
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uhispania Vicente del Bosque (61) ametangaza kikosi chake cha wachezaji 23 kitakachoiwakilisha Uhispania kwenye michuano ya Uefa Euro 2012 nchini Poland na Ukraine.

Kocha huyo wa kihispania amewaacha Adrian Lopez toka Atletico Madrid na Roberto Soldado toka Valencia huku akifanya mabadiliko ya wachezaji 9 baada ya kuwajumuisha kundini wachezaji toka Barcelona na Athletic Bilbao waliocheza fainali ya Copa del Rey siku ya Ijumaa.

Kuachwa kwa Adrian Lopez aliyeonyesha mchezo wa kuvutia kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Serbia pamoja na kuachwa kwa Soldado kumewashangaza wadau wengi wa soka nchini Spain na dunia kwa ujumla. 

Mapema mwezi huu Vicente del Bosque alinukuliwa akisema kuwa Pedro atabaki nyumbani akitazama michuano hiyo kwenye luninga, hali imekuwa tofauti baada ya kocha huyo kumjumuisha mshambuliaji huyo toka Fc Barcelona hasa baada ya kufunga magoli mawili kwenye fainali ya Copa del Rey dhidi ya Bilbao.

Uhispania watatupa karata yao ya kwanza kwenye michuano hiyo ya Euro 2012 dhidi ya Italia (june 10) kabla ya kucheza na Jamhuri ya Ireland (june 14) na baadae Croatia (june 18)

Kabla ya kuanza kwa michuano hiyo, mabingwa hawa wa Dunia na Ulaya watacheza tena michezo yao ya kirafiki dhidi ya Korea Kusini na Uchina.

KIKOSI CHA UHISPANIA KUELEKEA UERO 2012

JinaKlabu
Makipa: 
Iker CasillasReal Madrid
Pepe ReinaLiverpool
Victor ValdesBarcelona
Mabeki: 
Raul AlbiolReal Madrid
Jordi AlbaValencia
Alvaro ArbeloaReal Madrid
Sergio RamosReal Madrid
Juanfran TorresAtletico Madrid
Gerard PiqueBarcelona
Javi MartinezAthletic Bilbao
Viungo/Midfielders: 
Sergio BusquetsBarcelona
XaviBarcelona
Andres IniestaBarcelona
Xabi AlonsoReal Madrid
Santi CazorlaMalaga
Cesc FabregasBarcelona
David SilvaManchester City
Jesus NavasSevilla
Juan MataChelsea
Washambuliaji: 
PedroBarcelona
Alvaro NegredoSevilla
Fernando TorresChelsea
Fernando LlorenteAthletic Bilbao

YAJUE MAKUNDI YA MICHUANO YA EURO 2012

Group A

CountryWDLGDPts
Czech Rep.00000
Greece00000
Poland00000
Russia00000
 

 

Group B

CountryWDLGDPts
Denmark00000
Germany00000
Netherlands00000
Portugal00000

Group C

CountryWDLGDPts
Croatia00000
Italy00000
R. of Ireland00000
Spain00000

Group D

CountryWDLGDPts
England00000
France00000
Sweden00000
Ukraine00000