Pages

Friday, 12 July 2013

Brendan Rogers: Liverpool haitakiwi kumuuza Suarez anayewamiwa na Arsenal

Meneja wa klabu ya Liverpool amesisitiza kuwa timu hiyo haitakiwi kumuuza Luis Suarez anayewaniwa na Real Madrid pamoja na Arsenal.

Mchezaji huyo ambaye amekuwa akiongelea suara lake la kuhama kwenye timu hiyo karibu kipingi chote cha mapumziko ya ligi kuu yanayoendelea mpaka sasa amkekuwa akitakiwa na vilabu mbalimbali barani ulaya huku Real Madrid ikiwa ndiyo sehemu inayoonekana kumfaa zaidi mchezaji huyo mwenye miaka 26.

Hata hivyo kocha wa Arsenal mfaransa Arsene Wenger naye ameonekana kuvutiwa sana na mchezaji huyo kiasi cha kuwa na mpango wa kuongeza dau zaidi ya lile la paundi 30 elfu alilotuma mwanzao na kukataliwa na Liverpool.

Mchezaji huyo wa Uruguayi ameonekana na nia ya kutaka kuondoka klabuni hapo kwa kisingizio cha kuchoshwa na jinsi vyombo vya habari vya uingereza vinavyotaka kuuza kwa sababu ya kufuatilia maisha yake, lakini hivi karibuni mwakilishi wa mchezaji huyo alisema kuwa mchezaji huyo anataka kucheza kwenye timu inayoshiriki Champions Ligi msimu ujao.

"kwa miezi kadhaa sasa kumekuwa na hizi tetesi zikimhusisha Luis kuondoka Anfield lakini ukweli unabaki palepale kuwa Luis bado ni mchezaji wa Liverpool tunamjali na kutambua mchango wake kwenye timu iwapo uwanjan hata nje ya uwanja pia....nimeongea nae mara kwa mara kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno na kwa simu pia kuhusu tetesi hizi na ukweli unabaki palepale kuwa tunamheshimu sana Luis.." Brendan Rogers alikiambia kituo cha Radio cha TalkSPORT

Chelsea pia imeonekana kumwania mchezaji huyo ingawa kocha wa timu hiyo Jose Morinho ameonekana kuwekeza nguvu zake nyingi kwa mshambuliaji wa Kiingereza na timu ya Manchester United Wyne Rooney